Sport
Dollar
38,7692
0.02 %Euro
43,1659
-1.12 %Gram Gold
4.034,3300
-2.64 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kongamano hilo maalumu la kiuchumi, ambalo linaanza Mei 12 hadi 13, 2025, litawaleta pamoja jumla ya washiriki 2,000 kutoka pande mbalimbali za bara la Afrika.
Viongozi wa mataifa mbalimbali barani Afrika, wachumi na Maafisa Watendaji Wakuu wanakutana jijini Abidjan nchini Ivory Coast, kujadili hali ya uchumi wa bara hilo.
Kongamano hilo maalumu la kiuchumi, ambalo linaanza Mei 12 hadi 13, 2025, litawaleta pamoja jumla ya washiriki 2,000 kutoka pande mbalimbali za bara la Afrika.
Washiriki hao watajadiliana mambo mbalimbali yenye kuangazia nafasi ya sekta binafsi katika maendeleo ya bara hilo, wakati wa makala ya 12 ya kongamano hilo.
Tanzania itawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kongamano hilo, huku Rais Paul Kagame akishiriki kwa niaba ya Rwanda.
Viongozi wengine watakaoshiriki mkutano huo ni pamoja na Rais Mohamed Ould Ghazouani wa Mauritania, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Bassirou Diomaye Faye wa Senegal.
Comments
No comments Yet
Comment