Sport
Dollar
38,7681
0.01 %Euro
43,0066
-1.5 %Gram Gold
4.021,8200
-2.94 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mhalifu aliyekamatwa anaitwa Imanantireganya Alfadudu, maarufu kama “ MCongo”.
Idara ya polisi Uganda inasema imemkamata mmoja wa wahalifu sugu nchini.
Mhalifu huyo alikamatwa katika wilaya wa Wakiso ambayo inapakana na mji mkuu wa Kampala.
Mhalifu aliyekamatwa anaitwa Imanantireganya Alfadudu, maarufu kama “ MCongo.”
“Anashukiwa kuhusika katika msururu wa ujambazi na mauaji ya kukithiri katika eneo la Kampala, Busoga Mashariki, Busoga Kaskazini, eneo la Elgon, Ssezibwa, na maeneo jirani,” polisi ya Uganda imeeelezea.
“Wakati wa kuhojiwa na timu yetu ya usalama, Alfadudu alifichua kwamba yeye na washirika wake-waliotambuliwa kama Mozy, Mapengo, na wengine-walifanya ujambazi kwa kutumia bunduki ya SAR. Aidha alifichua kuwa kwa kawaida silaha hiyo ilifichwa katika makazi ya mtu anayeitwa Ivulungo Bumali katika Kijiji cha Girigiri,…Wilaya ya Mayuge, baada ya vitendo vyao vya uhalifu,” taarifa ya polisi ilielezea zaidi.
Idara ya Polisi inasema kufuatia taarifa hii, maafisa wa polisi na vyombo vya usalama walielekea Wilaya ya Mayuge, ambako walipata bunduki aina ya SAR kutoka kwa nyumba ya Ivulungo katika Kijiji cha Girigiri.
Vitu vya ziada vilivyokamatwa ni pamoja na nyundo mbili, kisu na jaketi.
Ivulungo na mkewe waliwekwa chini ya ulinzi ili kusaidia uchunguzi unaoendelea.
Matokeo ya awali yanadokeza kwamba bunduki iliyopatikana ilibiwa awali katika wizi Oktoba 2024.
Comments
No comments Yet
Comment