Dollar

38,7589

-0.04 %

Euro

43,6262

-0.2 %

Gram Gold

4.089,3800

-1.31 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Ibrahim Traore anataka ushirikiano zaidi wa kibiashara na teknolojia na amepongeza jukumu la kimataiffa la Urusi licha ya vikwazo vya Magharibi

Traore wa Burkina Faso ataka ushirikiano zaidi na Urusi

Rais wa Burkina Faso Ibrahim Traore amesema anataka ushirikiano wa nchi yake na Urusi

uwe “kielelezo” na ukue katika maeneo mapya.

“Ningependa ushirikiano kati yetu ukue na uchukue muundo mpya,” amesema Traore baada ya kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow.

Pia amehimiza umuhimu wa msaada wa teknolojia na kubadilishana uzoezi na Urusi.

“Tuna kazi kubwa mbele yetu. Na kitu kikubwa unachoweza kutusaidia nacho ni kubadilishana, ili kuhamisha teknolojia, uzoefu,” ameongeza kusema Traore akiwa Kremlin.

Msaada wa kibinadamu wa Urusi

Kwa upande wake, Putin, ameelezea ukuaji-ingawa wa kawaida-na kiwango cha biashara kati ya nchi mbili hizo.

“Bado inakuwa, na huu ni ukuaji mzuri. Tunahitaji kufanya kazi zaidi pamoja ili kukuza mafungamano ya kiuchumi na biashara za pamoja,” amesema.

Rais wa Urusi pia amegusia kuendelea kwa nchi yake kutoa misaada ya kibinadamu kwa Burkina Faso, licha ya kuwepo kwa vikwazo.

“Mwaka jana, tuliwatumia, tani 25,000 za ngano bure, na mwezi huu, shehena kubwa ya mazao ya chakula itafika Ouagadougou,” amesema.

Traore, akizungumzia jukumu la Moscow katika jukwaa la dunia, amesema: “Licha ya vikwazo vyote ambavyo Urusi imewekewa na baadhi ya nchi, Urusi inachukua nafasi muhimu katika uwanja wa kimataifa, na tunalizingatia hilo.”

Traore na baadhi ya viongozi wa Afrika waliwasili Moscow Mei 8 na kuhudhuria Gwaride la Ushindi katika Uwanja wa Red Square siku iliyofuata, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 80 ya Ushindi katika Vita Vikuu vya Uzalendo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#