Sport
Dollar
38,7786
0.39 %Euro
43,8944
0.27 %Gram Gold
4.147,5900
1.06 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021, Wine alikuwa wa pili, lakini alikataa matokeo, na kudai kulikuwa na wizi wa kura. Tuhuma ambazo serikali na Tume ya Uchaguzi ilizikana.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na msanii Bobi Wine, amesema Ijumaa kuwa ana mpango wa kugombea urais wa nchi hiyo kwa mara ya pili huku akizilaumu nchi za magharibi kwa kufumbia macho “ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu” anaodai unafanyika nchini mwake.
Wine, wenye umri wa miaka 43, ambae jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, kwa mara nyengine ataingia katika kinyang’anyiro hicho na mpinzani wake, ambae ni rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Yoweri Museveni, mwenye miaka 80. Wengi wanatarajia Rais Museveni atasimama tena.
“Ndio, nimeelezea kupatikana kwangu kwa niaba ya timu yangu,” amenukuliwa Wine katika mahojiano na Reuters pindi alipoulizwa iwapo ana nia ya kusimama tena katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, ambao unatarajiwa kufanyika Januari, 2026.
Kushiriki katika uchaguzi, amesema Wine, pia itakuwa ni “fursa ya kupambana na kuuanika uongozi na kuunganisha watu wa Uganda kusimama ili kujipatia huru wao.”
Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021, Wine alikuwa wa pili, lakini alikataa matokeo, na kudai kulikuwa na wizi wa kura. Tuhuma ambazo serikali ilizikana.
Comments
No comments Yet
Comment