Sport
Dollar
38,7786
0.39 %Euro
43,8944
0.27 %Gram Gold
4.147,5900
1.06 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Serikali mpya ya gavana wa M23 kwenye mkoa wa Kivu ya Kusini inasema kampuni ya uchimbaji madini ya Twangiza Mining lazima ifuate sheria mpya na kulipa kodi ambazo zinadaiwa walikuwa hawalipi.
Twangiza Mining, kampuni inayochimba madini ya dhahabu iliyopo katika eneo linalodhibitiwa na waasi mkoa wa Kivu Kusini huko mashariki mwa DRC, inasema imetakiwa kusitisha shughuli zake na uongozi huo wa waasi, kulingana na barua waliyosambaza na ambayo imeonekana na shirika la habari la Reuters.
Kampuni hiyo, ambayo inasimamiwa na shirika lililosajiliwa Hong Kong- la Shomka Resources, iliwafahamisha wafanyakazi kuhusu kusimamisha shughuli katika barua hiyo iliyoandikwa 8 Mei.
"Kufuatia maagizo ya utawala mpya ulioko Mkoa wa Kivu Kusini, Twangiza Mining imelazimika kusitisha shughuli zake," barua hiyo iliyotiwa saini na Mkurugenzi Mkuu Chao Xianfeng inasema, ikiongeza kuwa mashine na magari hazitotumika kwa sasa.
Uamuzi huu unadhihirisha mvutano kuhusu udhibiti wa raslimali katika maeneo yenye utajiri wa madini mashariki mwa Congo, ambapo utawala mpya wa waasi wa M23 umechukua udhibiti wa raslimali za kimkakati, na kuzua taharuki kwa wachimbaji madini wa kimataifa na bei ya madini hayo.
Maeneo yaliyodhibitiwa
Waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda walichukua udhibiti wa mikoa miwili yenye utajiri wa madini ya mashariki mwa Congo mwaka huu, na wanaendeleza udhibiti wao zaidi.
Manu Birato, ambaye hivi karibuni aliteuliwa gavana wa M23 wa mkoa wa Kivu Kusini, anasema Twangiza Mining lazima ifuate sheria mpya na kulipa kodi ambazo wamekuwa hawalipi.
"Tunazungumza nao na kuwaeleza kuwa kuanzia sasa lazima walipe kodi," Birato aliambia Reuters.
"Nchi hii haijapata kodi yoyote kutoka kwa hiyo kampuni. Pesa zimeenda kwenye mifuko ya watu binafsi," alisema, akiongeza kuwa uongozi haujaamuru kuwa mgodi ufungwe.
"Tumewaambia waanze kulipa kodi. Wanapata tabu kufuata hizi sheria mpya, kutokana na kuwa walikuwa hawalipi chochote," Birato amesema.
Msemaji wa kampuni ya Twangiza alikataa kujibu kuhusu madai ya Birato.
Kampuni ya Twangiza Mining ni ubia kati ya kampuni ya Congo, Shomka Capital yenye 65.5% ya hisa, na kampuni ya China Baiyin International Investments Ltd, ambayo ina 34.5% ya hisa.
Comments
No comments Yet
Comment