Sport
Dollar
38,7786
0.39 %Euro
43,8944
0.27 %Gram Gold
4.147,5900
1.06 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Haya yanajiri baada ya Marekani kusitisha msaada wa dola milioni 50 wa kila mwaka kwa masuala ya matibabu kutokana na uwizi wa dawa na usaidizi mwingine, dawa ambazo zilitakiwa kutolewa bure
Wizara ya afya ya Zambia inasema inachukua hatua dhidi ya uwizi wa dawa zilizotakiwa kutolewa bure baada ya Marekani kutangaza kukata msaada mkubwa kutokana na serikali kushindwa kukabiliana na tatizo hilo.
Siku ya Alhamisi Marekani ilitangaza kuwa itasitisha msaada wa dola milioni 50 kila mwaka katika masuala ya afya nchini Zambia kufuatia uwizi wa dawa na usaidizi mwingine ambao ulitakiwa kutolewa bure kwa watu wasiojiweza lakini dawa zikapatikana zikiuzwa katika maduka ya dawa.
Kama njia ya kujibu kuhusu sakata hilo Alhamisi jioni, Waziri wa Afya wa Zambia Elijah Muchima alikiri kuwa: "Uwizi wa dawa unaathiri utoaji huduma ya matibabu kwa umma, na kuwanyima wagonjwa matibabu muhimu, pamoja na kufanya watu kutokuwa na imani na mfumo wa afya wa Zambia."
"Changamoto hii ambayo imekuwepo ni ishara ya tatizo kubwa sana," alisema.
Maafisa wasimamishwa kazi
Hatua za kuzuia uwizi huo zimechukuliwa, ikiwemo kusimamishwa kazi au kufutwa kwa maafisa waandamizi waliohusishwa na sakata hilo, alisema.
Ubalozi wa Marekani umesema kuwa uwizi huo uligunduliwa mwaka 2021 lakini serikali ilikuwa imewakamata maafisa wa ngazi ya kati tu kwa kuhusika na wala siyo maafisa wakuu waliofaidika zaidi.
Wizara ya Afya imesmea kuwa ukaguzi huru wa mahesabu pia ulichangia kuwafuta kazi maafisa waandamizi wa shirika la kusambaza dawa, ikiwemo Mkurugenzi Mkuu, na hatua zingine zinatarajiwa kufuata.
"Hatutamuacha mtu yeyote kutokana na umuhimu wake katika mchakato huu," Muchima alisema.
Kutegemea misaada
Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika yenye idadi ya watu milioni 21 inategemea sana misaada kutoka nje. Karibu thuluthi moja ya matumizi yake ya umma inatoka Marekani, hii ni kulingana na taarifa kutoka Marekani.
Wizara ya afya imetaka kuondoa hofu kuwa kwa sasa kuna uhaba wa dawa kufuatia kusitishwa kwa misaada ya Marekani, ikisema kuwa bado ina kiwango cha asilimia 75 ya dawa za kutibu malaria, HIV na kifua kikuu.
Zaidi ya asilimia 64 ya watu katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika yenye utajiri wa madini ya shaba wanaishi katika hali ya umaskini, kutokana na miaka mingi ya ufisadi unaotekelezwa na watu wachache wenye ushirikiano na wanasiasa.
Comments
No comments Yet
Comment