Dollar

38,7786

0.39 %

Euro

43,8944

0.27 %

Gram Gold

4.147,5900

1.06 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Kenya, William Ruto, amemteua Erastus Edung Ethekon kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka – IEBC, pamoja na makamishna sita wapya.

Erastus Edung Ethekon Mwenyekiti mteule wa tume huru ya uchaguzi Kenya ni nani?

Tume hiyo imekuwa bila uongozi kwa zaidi ya miaka miwili, hali iliyozua wasiwasi kuhusu uwezo na utayari wa nchi hiyo kuandaa uchaguzi.

Ethekon, mwenye umri wa miaka 48, pamoja na watakao kuwa makamishna wa tume hiyo hivi sasa wanasubiri hatua ya kujadiliwa na bunge kabla kuidhinishwa.

Iwapo atapitishwa, basi Ethekon atakuwa na jukumu kubwa la kuanza kuisuka upya  na kuiongoza IEBC katika kipindi muhimu cha uchaguzi. 

Kwa zaidi ya miaka ishirini, Ethekon amehudumu kama mshauri katika masuala ya sheria na maendeleo kupitia kampuni za Northern Consulting Solution na Ethekon & Co. Advocates.

Kazi yake kitaaluma ilianza mwaka 2007 katika Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa – UNDP kama mtaalamu wa miradi, baadaye alihamia nafasi ya mshauri wa miradi katika shirika hilo hilo.

Mwaka 2018, aliteuliwa kuwa Mwanasheria wa Kaunti ya Turkana, nafasi aliyohudumu kwa miaka sita. 

Kitaaluma, Ethekon ana shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, stashahada ya uzamili ya sheria kutoka Kenya School of Government, na cheti cha haki za binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Nottingham, Uingereza.

Pia ana shahada tatu za uzamili: Masuala ya Amani, Migogoro na Maendeleo kutoka Universidad Jaume I nchini Uhispania (2012), Usimamizi wa Miradi kutoka Chuo Kikuu cha Liverpool, Uingereza, na Masuala ya Sheria ya Mafuta na Nishati kutoka Chuo Kikuu cha Derby, Uingereza. 

Ni nafasi ambayo, imekuwa na utata mkubwa kwa watangulizi wake, huku wakituhumiwa kwa upendeleo, tuhuma ambazo hazikuwahi kuthibitishwa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#