Sport
Dollar
38,7786
0.39 %Euro
43,8944
0.27 %Gram Gold
4.147,5900
1.06 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Katika kipindi hiki kigumu, Umoja wa Ulaya uliyo thabiti ni muhimu kwa maslahi ya kila mtu, amesema Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amepongeza watu wa Ulaya katika siku ya kuadhimisha Siku ya Ulaya 9 Mei.
Kulingana na taarifa kupitia mtandao wa kijamii wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, Rais Erdogan, katika ujumbe wake wa pongezi, alieleza kuwa siku ya Ulaya ni ishara ya mchakato wa kuunganisha Ulaya katika masuala ya siasa na uchumi, ambao ulianza na Azimio la Schuman la 1950.
Akisisitiza kuwa EU, ni ishara ya ushirikiano wa Ulaya, na kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na changamoto duniani na katika kanda yake katika miaka ya hivi karibuni, Erdogan amesema: “Mustakabali wa muundo wa usalama wa Ulaya unajadiliwa; kuwa kimya kuhusu mauaji ya kikatili huko Gaza kwa miezi 19 na kushindwa kuunda sera thabiti ya kuzuia mashambulizi ya Israeli inafanya watu wahoji kuhusu maadili ya Umoja huo.”
Akieleza kuwa EU ya sasa inahitaji mtazamo thabiti na dira nzuri, Erdogan alisema: "Katika kipindi hiki kigumu, ushirikiano wa Umoja wa Ulaya ambao hauna ubinafsi wa kuangalia maslahi ya nchi mmoja, lakini wenye kuangazia maslahi ya pamoja bara zima, ni jambo lenye maslahi kwa kila mtu. Nchi yetu, ambayo inasubiri uanachama wa EU licha ya kukabiliwa na vizingiti, pia inaonesha umuhimu wa Umoja wa Ulaya kuwepo pamoja na sera zake za ubinadamu, amani na sera zenye kuleta tija na kutafuta suluhu ya haki kwa mizozo na mapigano."
"Ukweli ni kuwa, matukio ya hivi karibuni duniani, ambayo yameathiri ulimwengu mzima na kusababisha kuangaliwa upya kwa sera zilizokuwepo, kwa mara nyingine yameonesha umuhimu wa uhusiano wa Uturuki na Umoja huo,” amesema.
“Licha ya kuwepo kwa mtazamo usio wa haki kwa baadhi ya watu na makundi yanayodai kuwakilisha taasisi ya Umoja wa Ulaya dhidi ya nchi yetu mara kwa mara,” Erdogan anasema bado anaamini kuwa EU “itaonesha busara ya kuchukua hatua yenye mtazamo wa muda mrefu na ya kimkakati kwa faida ya wote katika kipindi kinachokuja.
Katika kuadhimisha siku hii, nawapongeza watu wa Ulaya, haswa raia wangu wenyewe, katika Siku hii ya Ulaya."
Comments
No comments Yet
Comment