Dollar

38,5992

0.33 %

Euro

43,6545

0.2 %

Gram Gold

4.017,2800

0.33 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Uturuki Erdogan aelezea dhamira ya Uturuki kwa mustakbali, akisisitiza umuhimu a TeknoFest na miradi ya kimkakati katika ukuaji wa Jamhuri ya Uturuki ya Kopru ya Kaskazini.

Erdogan atangaza Uturuki miongoni mwa tatu bora katika teknolojia ya UAV katika tamasha la TeknoFest

 Katika hotuba aliyoitoa katika Sherehe za Kutoa Tuzo za TEKNOFEST katika eneo la Lefkosa Jumamosi, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza kwamba Uturuki iko katika orodha ya nchi tatu duniani katika teknolojia ya ndege zisizotumia rubani (UAV).

Ameahidi kuendelea katika nyanja hiyo kwa ari na dhamira kuu.

Erdogan ameonyesha matumaini ya maisha ya yajao, na kuongeza, “Kuwepo kwa vijana TEKNOFEST, miradi inayokuwa TRNC, na jitihada zetu za kimkakati, tutaendelea kusimama hapa kwa karne zinazokuja.”

“Sisi kama taifa la Uturuki na Uturuki ya Kopru, ndio wenye ardhi hii. Wale wasiojua, sharti wajue, na wale ambao hawajasikia, sharti wasikie,” Erdogan alitangaza, akisisitiza uhusiano imara wa Uturuki na Jamhuri ya Uturuki ya Kopru Kaskazini (TRNC).

Nae Rais wa TRNC Ersin Tatar, kwa upande wake, pia alipongeza mafanikio ya sekta ya ulinzi ya Uturuki, na kusema, “Mafanikio ya taasisi za Uturuki katika sekta ya ulinzi ni fahari ya dunia yote ya kituruki.”

Maonyesho ya Uturuki ya teknolojia, anga, TEKNOFEST, yamefanywa TRNC na kuvutia maelfu ya watu katika eneo la Lefkosa, ambapo takriban ya wageni 62,000 wamehudhuria siku ya kwanza ya maonyesho hayo ya siku nne.

Maonyesho hayo yameratibiwa na taasisi ya Uturuki ya Teknolojia (T3) na Wizara ya Viwanda na Teknolojia. TEKNOFEST ni tukio la kila mwaka tangu 2018 huku likiungwa mkono na taasisi mbalimbali za serikali, sekta binafsi na vyuo vikuu.

Maonyesho hayo yanafanyika maeneo mbalimbali katika miji ya Uturuki katika miaka yenye namba zinazogawanyika, na hufanyika jijini Istanbul katika miaka isiyogawanyika, huku TRNC ikiwa mwenyeji wa pili wa kimataifa baada ya Azerbaijan, ambayo ilihodhi TEKNOFEST katika toleo lake la 10.

Mwaka 2024, TEKNOFEST ilivutia takriban wageni milioni 1.1 katika mji wa kusini wa Adana.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#