Dollar

38,6139

0.11 %

Euro

43,6588

-0.13 %

Gram Gold

4.171,0600

0.89 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Erdogan na Trump wamejadili masuala ya kikanda na dunia katika mazungumzo yao kwa njia ya simu.

Erdogan aashiria ushirikiano mkubwa katika masuala ya ulinzi na Marekani

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitiza dhamira ya Uturuki kuimarisha ushirikiano na Marekani, hasa katika eneo la ulinzi, kwenye mazungumzo kwa njia ya simu na rais wa Marekani Donald Trump.

Viongozi hao wawili walijadiliana masuala kadhaa, ikiwemo uhusiano wa Uturuki na Marekani, masuala ya kikanda na yanayoendelea duniani, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki ilisema katika taarifa kwenye mtandao wa X siku ya Jumatatu.

Wakati wa mazungumzo hayo kwa njia ya simu, Erdogan alieleza kuunga mkono hatua ya Trump ya kutaka kumaliza vita na kueleza kuridhika kwa juhudi za kuanza tena majadiliano na Iran, pamoja na juhudi za kumaliza vita vya Urusi na Ukraine, taarifa hiyo ilisema.

Akizungumzia kuhusu hali mbaya kwa watu wa Gaza, Erdogan alisisitiza kuhusu mateso wanayopitia watu wa Gaza na kusisitiza lazima misaada iruhusiwe kuingia huko bila vikwazo vyovyote.

Kauli ya Trump ilikuwa ni kujibu kuhusu Tom Barrack, Balozi mteule wa Marekani nchini Uturuki, ambaye alieleza umuhimu wa kihistoria wa nchi hiyo.

Ushirikiano katika kupatikana kwa amani ya kudumu

Erdogan amesema Uturuki iko tayari kushirikiana na kutoa msaada wowote unaohitajika ili kuhakikisha vita vimesitishwa na kupatikane amani ya kudumu, taarifa iliongeza.

Erdogan alisisitiza pia kujitolea kwa Uturuki kuhakikisha kuwa uhuru wa mipaka ya Syria unaheshimiwa na kuhakikisha utulivu katika nchi hiyo. Alieleza kuwa juhudi za Marekani za kuondoa vikwazo kwa Syria huenda zikachangia katika kuleta amani katika kanda na dunia.

Rais Erdogan pia alimualika Trump kutembelea Uturuki, taarifa hiyo ilisema.

Trump alieleza mazungumzo hayo kuwa "mazuri na yenye tija" na kusema kuwa anatarajia kufanya kazi na Rais wa Uturuki katika kumaliza vita vya Urusi na Ukraine.

Pia alitangaza kuwa Erdogan “atakuja Washington, DC”.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#