Dollar

38,5992

0.33 %

Euro

43,6545

0.2 %

Gram Gold

4.017,2800

0.33 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Waandishi wa habari wa kimataifa wanaoendesha baiskeli wamesifu Ziara ya Rais wa Baiskeli ya Uturuki ya miaka 60 kama tukio la aina yake katika jukwaa la kimataifa.

Waandishi wa habari wasifia Ziara ya Uturuki ya mbio za baiskeli

Waandishi wa habari wa kimataifa wamesifu Ziara ya Uturuki kama moja wapo ya tukio kubwa duniani kwa waendesha baiskeli

Mbio hizo, zilizoanza Antalya zimekamilika Jumapili katika kituo cha mwisho kutoka Cesme mpaka Izmir.

Waandishi wa habari wa kimataifa wanaoendesha baiskeli wamesifu Ziara ya Rais wa Baiskeli ya Uturuki ya miaka 60 kama tukio la aina yake katika jukwaa la kimataifa.

Sander Kolsloot, mhariri mkuu wa Hetiskoers.nl, ameiambia Anadolu kwamba kwa miaka mingi amefuatilia Ziara hiyo, lakini hii ni mara ya kwanza kuifuatilia kwa karibu zaidi.

“Inachangamsha, na nadhani ni ziara nzuri. Unaweza kuona hilo katika kiwango cha washiriki,” amesema.

Kolsloot amesema sehemu anayoipenda katika ziara hiyo ni Kituo cha 4.

“Ni sehemu nzuri ya kushuhudia shindano. Naamini Kituo cha 4 kitakuwa katika Mlima wa Kiran.”

Kolsloot amehimiza kwamba Ziara ya Uturuki haiwezi kulinganishwa na mashindano ya mbio za baiskeli ya Tour de France, lakini kwa ujumla, mashabiki “wana ari na furaha. Kwa hiyo hilo ni jambo zuri kuona.”

“Kiwango kinazidi kuwa bora,” amesema.

‘Mazingira yanapendeza’

Mwandishi mwengine muendesha baiskeli, Jens Voegele, ambae anafanya kazi katika taasisi ya habari ya Ujerumani, Westsider, amesema kama muendesha baiskeli amevutiwa na mabadiliko ya shindano hilo.  Jinsi linavyoratibiwa, viwango vya washiriki na jinsi waendeshaji wanavyovuka hatua moja hadi nyengine.

“Watu wanashauku kubwa ya shindano. Kwa hiyo, ni vyema kuwa hapa na kupata hisia ya shindano,” amesema Voegele.

Mwandishi wa habari wa Italia Filippo Lorenzon, ambae anafanya kazi Bici.pro na Bici.style, amesema ameona watu wengi wakiwa pembezoni mwa barabara na bendera nyingi za Uturuki.

Lorenzo amesema alifurahia chai ya Uturuki.

“Nimependa harufu nzuri na ladha ya hapa. Kesho asubuhi, natarajia chai ya asubuhi inayofanana-itakuwa nzuri!” amesema.

Alejandro Adrian Lingenti kutoka Cisclosfera, Uhispania, amesema hii ilikuwa ni mara yake ya pili kuandika habari za Ziara ya Uturuki.

“Watu ni wakarimu, mazingira mazuri, na shindano lenyewe ni zuri,” amesema.

“Ni nchi nzuri kwangu. Nikiwa natoka Uhispania, ni tofauti kabisa.”

Washiriki wa shindano hilo wameendesha baiskeli kilomita 1,153 (maili 716) katika hatua nane ambazo zimeanza Jumapili iliyopita Antalya, wameendesha katika maeneo maarufu ya kitalii kama vile Kemer, Kalkan, Fethiye, Marmaris, Ankyaka, Aydin, Kusadasi, Selcuk na Cesme kabla ya kufika eneo la mwisho la Aegean Mei 4 katika mji wa Izmir.

 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#