Dollar

38,5992

0.33 %

Euro

43,6545

0.2 %

Gram Gold

4.017,2800

0.33 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Ankara imekosoa shambulizi dhidi ya chombo hicho kilichokuwa kinamilikiwa na Umoja wa Uhuru wa Flotilla.

Uturuki yalaani shambulizi dhidi ya meli ya Flotilla

Uturuki imelaani shambulizi dhidi ya meli iliyokuwa ikimilikiwa na Umoja wa Uhuru wa Flotilla, kikundi ambacho kilipaza sauti ya watu wa Gaza, wanaokabiliwa na baa la njama, huku Israeli ikiendeleza kuzuia kupitishwa kwa misaada ndani ya eneo hilo la Palestina.

Kulingana na Ankara, shambulizi hilo ni tishio kwa usalama wa usafiri wa majini.

Ikiwa na abiria 16, chombo hicho kilichokuwa kikielekea Gaza, kilishambuliwa na ndege nyuki na kuharibika vibaya.

Hata hivyo, waliokuwa ndani ya chombo hicho waliokolewa na vikosi vya Maltese.

Shambulizi hilo lilisababisha kukatika kwa umeme ndani ya meli na kukiweka chombo hicho kwenye “hatari ya kuzama,” ilisema sehemu ya taarifa iliyotolewa na umoja huo ambao umeazimia kumaliza zuio la uingizwaji wa misaada ndani ya Gaza.

“Katika majira ya nane na dakika kumi na tatu alfajiri, ilithibitika kuwa wote waliokuwa ndani ya chombo hicho walikuwa salama, lakini hawakuwa tayari kuiacha meli hiyo,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa hali ya kawaida ilirejea ilipofika saa tisa na dakika 45 asubuhi.

Kwa sasa, chombo hicho kinachokulikana kama Conscience, kipo katika eneo la kimataifa la bahari, chini ya uangalizi wa mamlaka.

Licha ya kuwa, hakuna aliyekiri kuhusika na tukio hilo, taasisi hiyo iliinyooshea Israeli kidole cha lawama.

“Israeli inalenga kuzishambulia meli za misaada kwa nia ya kuwaweka Wapalestina kwenye baa la njaa kama mbinu ya kivita,” ilisema taarifa hiyo ambayo ilimnukuu Dkt. Shahd Hammouri kutoka Chuo Kikuu cha Kent.

Kupitia ukurasa wa X, mtunza kumbukumnbu maalumu wa Palestina ndani ya Umoja wa Mataifa, Francesca Albanese, alisema kuwa alipata simu ya dharura kutoka kwa abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo.

"Natoa wito kwa wahusika wote kuisaidia meli pamoja na abiria wake," alisema.

Aliongeza: "Naziamini mamlaka hizo."

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#