Sport
Dollar
38,5992
0.33 %Euro
43,6545
0.2 %Gram Gold
4.017,2800
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Katika taarifa yake aliyoiweka kwenye mtandao wa X, Altun aliipongeza TRT, akiita “sauti ya nchi yetu na kumbukumbu ya taifa letu,” akilipongeza shirika hilo kwa kazi yake ndani ya miaka 60.
Fahrettin Altun aliipongeza TRT kwa kupaza sauti ya Uturuki ulimwenguni, akisisitiza kuwa shirika hilo limekuwa mjumbe muhimu wa Uturuki katika kupatikana kwa haki kimataifa na maono yake yake mawasiliano.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun amelipongeza shirika la habari la Uturuki TRT wakati likitimiza miaka 61, akielezea umuhimu wa taasisi katika jitihada za Uturuki za kusaka ukweli, kumbukumbu ya taifa na jitihada za mawasiliano.
Katika taarifa yake aliyoiweka kwenye mtandao wa X, Altun aliipongeza TRT, akiita “sauti ya nchi yetu n kumbukumbu ya taifa letu,” akilipongeza shirika hilo kwa kazi yake ndani ya miaka 60.
“Si tu kuhabarisha watu kupitia uzoefu wake wa miongo mingi, pia imesimamia ukweli, na kuwa daraja muhimu la mawasiliano kati ya watu na nchi yao,” alisema Altun.
Aliangazia nafasi ya TRT katika kukuza sauti ya Uturuki ulimwenguni, akisema kuwa shirika hilo limekuwa mjumbe muhimu wa Uturuki katika upatikajani wa haki kimataifa na maono yake kupitia mawasiliano.
“Kufikia leo, TRT sio chombo cha kawaida cha habari,” alisema Altun , “bali ni mfano wa chombo cha mawasilino cha Uturuki, chenye kutoa kipaumbele kwenye ukweli na mitazamo mbalimbali.”
Pia, aligusia maono ya Rais Recep Tayyip Erdogan maarufu kama “Karne ya Uturuki”, akiongeza kuwa shirika hilo lina nafasi muhimu katika kuimarisha uwepo wa Uturuki kimataifa.
Kama sehemu ya mkakati wa mawasiliano wa Uturuki, Altun ameahidi kuendelea kuimarisha uwezo wa kitaasisi wa TRT, uzalishaji wake na ufukiaji wake kimataifa.
Akihitimisha pongezi zake, Altun alishukuru wafanyakazi wa sasa na wale wa zamani wa TRT, akiitakia taasisi hiyo kila la heri katika safari yake ya utangazaji.
Comments
No comments Yet
Comment