Dollar

38,5992

0.33 %

Euro

43,6545

0.2 %

Gram Gold

4.017,2800

0.33 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Wizara ya Mambo ya Nje imeonyesha mpango wa Uturuki kuelekea utulivu wa kanda, katika kupambana na ugaidi, na ushirikiano mpya na Damascus.

Ankara inataka Syria kuungwa mkono kipindi cha mpito na kuondolewa vikwazo

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imetoa taarifa ya kina ikitaka uungwaji mkono wa kikanda na kimataifa wakati Syria ikiwa katika kipindi cha kisiasa cha mpito na kujijenga upya, kufuatia kile ilichokiita “kipindi kipya” katika historia ya nchi baada ya kuanguka kwa utawala wa Assad.

Taarifa ya Alhamisi imesisitiza kwamba watu wa Syria wanapambana kukabiliana na mateso ya mgogoro wa miaka 14 na ni lazima wawezeshwe kutengeza maisha yao ya baadae kupitia mchakato wa kisiasa unaoongozwa na Wasyria wenyewe.

Ankara imesisitiza kwamba hatua za hivi karibuni za Syria za kutaka kuwa sehemu ya diplomasia ya kikanda na kimataifa sharti iungwe mkono.

Imetahadharisha kwamba, kuendelea kutengwa na vikwazo inaweza kuhatarisha utulivu uliopo, na kuongeza kusema kwamba ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi, ikiwemo kuondoa vikwazo, ni muhimu kwa amani ya kudumu.

Uturuki imeweka hili kama mkakati muhimu wa kibinadamu, na kusema kuwa njia pekee ya kukabiliana na hali ya kutokuwa na usalama ni kupitia “msaada zaidi na ushirikishwaji.”

Mtizamo wa Uturuki Syria: Umoja, ulinzi na kujengwa upya

Uti wa mgongo wa sera ya Uturuki kwa Syria, kwa mujibu wa taarifa, unajikita katika kuhifadhi mipaka, kuondoka tishio la ugaidi, kufanikisha maridhiano ya kitaifa, na kuunga mkono ujenzi mpya kupitia kuondolewa kwa vikwazo.

Taarifa hiyo imeonyesha kupungua kwa shughuli za kijeshi kusini mwa Syria, ambapo vikosi vya wapiganaji vinaripotiwa kuingizwa katika jeshi jipya la taifa. Hata hivyo, imethibitisha kwamba, bado kuna mapigano, mara nyingi yanayosababishwa na uchokozi.

Hali ya wasiwasi kufuatia vitendo vya kigaidi vya YPG/PYD

Uturuki imeonyesha wasiwasi kuhusu uhusiano kati ya serikali ya Syria na YPG/PYD, ikugusia makubaliano yaliyotiwa saini kati ya pande mbili hizo.

Pia imekosoa mkutano uliofanywa na shirika la kigaidi la YPG/PYD katika eneo la Qamishli Aprili 26, na kusema ujumbe uliotolewa ulienda kinyume na makubaliano na SDF ya Damascus.

Ankara imesisitiza kuunga mkono umoja wa Syria na kuonya dhidi ya mpango wowote wenye ajenda ya kutenganisha.

YPG/PYD sehemu ya shirika la kigaidi la PKK nchini Syria, ambalo linahusika na zaidi ya vifo vya watu elfu 40 ikiwemo raia, pamoja na watoto.

Katiba mpya ya Syria lazima ilete usawa

Uturuki imehimiza kwamba muskabali wa Syria lazima ujengwe katika serikali jumuishi.

Inatarajia katiba yoyote mpya ya Syria kuleta usawa kwa matabaka yote na makundi ya kidini.

Wizara ya Mambo ya Nje imesema inapinga mfumo wowote ambao utazuia uhuru wa Wasyria wa kujieleza, na kwamba hatua yoyote ya kuzuia usawa itapingwa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#