Sport
Dollar
38,5992
0.33 %Euro
43,6545
0.2 %Gram Gold
4.017,2800
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Waziri anayesimamia masuala ya mafuta na madini nchini Somalia anasema ana imani kuwa ushirikiano huo utathibitisha uwezo wa upatikanaji wa gesi hiyo kwa ajili ya biashara.
Na Nuri Aden
Waziri wa Madini wa Somalia, Dahir Shire Mohamed, amepongeza ushirikiano mpya wa nchi yake na Uturuki katika suala la gesi ya haidrokaboni kama ulokuja “kwa wakati muafaka” wenye lengo la kutoa fursa ya kibiashara kwa raslimali hizo za asili.
Amesema hayo wakati wa kongamano la Raslimali za Asili lililofanyika jijini Istanbul (INRES 2025), mkutano wa ngazi ya juu, ambao umewaleta pamoja watunga sera, viongozi katika sekta za biashara, wafadhili na wabunifu katika masuala ya nishati kutoka kote duniani.
Katika mahojiano na TRT Afrika, waziri huyo alisisitiza dhamira ya Somalia kuondoa vizuizi ambavyo kihistoria vimekuwa kizingiti katika uchimbaji na uwekezaji kwenye raslimali za asili za nchi.
“Somalia ina utajiri wa raslimali ya madini na gesi ya haidrokaboni, lakini sehemu kubwa ya raslimali hizo bado hazijatumika vizuri kutokana na changamoto nyingi,” alisema Mohamed.
Muswada wa Madini
“Tunatoa kipaumbele kwa mabadiliko ya kisheria na kuwahamasisha wawekezaji. Kuna Muswada wa madini, ambao kwa sasa umefikishwa bungeni. Ukiidhinishwa, utatoa fursa ya kushirikiana vizuri na wawekezaji katika sekta yetu ya uchimbaji wa raslimali za asili.”
Ikiwa sehemu ya msingi ya ushirikiano kati ya Uturuki na Somalia, Uturuki imetuma meli yake ya utafiti ya Oruç Reis katika Bahari Hindi. Meli hiyo inafanya utafiti wa kiwango cha 3D katika bahari ya pwani ya Somalia, ni jambo ambalo halijawahi kufanyika katika historia ya uchimbaji mafuta na gesi nchini Somalia.
“Uturuki ndiyo taifa pekee ambalo limechukuwa hatua madhubuti za kukabiliana na changamoto zinazohusiana na raslimali za asili.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Uturuki, meli ya Utafiti ya Uturuki Oruç Reis imetoka Bahari Nyeusi na maeneo ya bahari ya Uturuki na kwenda sehemu ya nje, sasa hivi ikifanya tathmini kwa kutumia teknolojia ya 3D katika maeneo ya pwani ya Somalia kwenye Bahari Hindi,” Mohamed alieleza.
“Tuna matumaini kuwa mchakato huu utathibitisha kuwepo kwa raslimali ambazo zinawea kutumika kwa ukubwa katika kwa biashara,” aliongeza.
Hofu ya usalama
Somalia imekuwa katika vita kwa miongo kadhaa dhidi ya makundi ya wapiganaji katika nchi hiyo na waziri huyo alisema kushughulikia suala la usalama ni sehemu ya juhudi zinazofanyika ili tuwe na mazingira mazuri kwa wawekezaji.
“Ni muhimu sana kuwa na mazingira mazuri. Usalama ni kitu cha kwanza kwa makampuni yanayotaka kufanya shughuli za uchimbaji nchini Somalia,” amesema.
Lengo la nchi hiyo ni kujiunga na mataifa yanayouza mafuta nje ya nchi, ikiwemo uwanachama wa Jumuiya za mataifa hayo kama OPEC.
“Hiyo ndiyo dira yetu - kuona Somalia inakuwa moja ya nchi inayotegemewa katika kuuza nishati nje ya nchi,” alisema.
Alithibitisha kuwa Somalia ina mkataba mwingine wa uchimbaji na Uturuki, kusisitiza kuimarika kwa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili wenye lengo la kukuza utajiri wa raslimali wa Somalia.
“Somalia imesubiri kwa muda mrefu. Lakini sana, kwa ushirikiano wa uhakika na teknolojia ya Uturuki, tuko tayari kubadilisha utajiri wetu wa raslimali na kuwa mafaniko kwa taifa,” alisema.
Comments
No comments Yet
Comment