Sport
Dollar
38,6055
0.02 %Euro
43,6532
-0.23 %Gram Gold
4.133,5100
-0.02 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa Ghana amewaonya zaidi ya mawaziri wake 40 na wateule wengine kwa kushindwa kuweka wazi mali wanazomiliki, huku muda wa mwisho wa kufanya hivyo ukitarajiwa kuwa Jumatano, 7 Mei.
Siku ya Jumatatu rais wa Ghana amesema kuwa amewaonya mawaziri na wateule wengine zaidi ya 40 kuhusu kushindwa kuweka wazi mali wanazomiliki, wakati kiongozi huyo mpya akiendelea na vita dhidi ya ufisadi.
Tangu kuapishwa kwake mwezi Januari, Rais John Mahama ameahidi kukabiliana na ufisadi wakati akijaribu kuimarisha uchumi wa nchi.
Mwezi Aprili, mamkala zilimshtaki afisa mmoja mwandamizi wa zamani wa usalama kwa ubadhirifu wa kupokea mamilioni ya dola kupitia kandarasi ya usalama wa mitandaoni.
Hata hivyo hatua ya Jumatatu inaonekana kama kali zaidi kwa Mahama aliyezindua kanuni ya maadili kwa wafanyakazi wa serikali.
'Kufutwa kazi mara moja'
Wale watakaobainika kwenda kinyume na tarehe ya mwisho ya kuweka wazi mali wanazomiliki kufikia Jumatano, ambayo awali ilikuwa 31 Machi, hawatopokea mshahara wa miezi minne – mitatu kama adhabu na wa mwezi mmoja kuchangia kwa lazima mradi wa mfuko mpya wa kusaidia masuala ya matibabu, maarufu nchini Ghana kama "Mahama Cares".
"Kama kufikia mwisho wa siku ya Jumatano, 7 Mei, 2025, yeyote kati yenu ambaye atakuwa hajaweka wazi mali anazomiliki, fahamu mara moja kuwa umeshafutwa kazi," rais alisema katika hotuba yake mjini Accra.
Kanuni mpya za maadili ni kwa wateule wote wa kisiasa, ikiwemo mawaziri, manaibu waziri, wafanyakazi wa ofisi ya rais na Mahama mwenyewe.
Ufisadi katika utumishi wa umma umekithiri siyo tu kwa Ghana peke yake lakini kwa kanda nzima.
Onyo 'si la mzaha'
Madai ya ufisadi yalizonga muhula wa kwanza wa Urais wa Mahama kuanzia 2012 hadi 2017, ingawa hakuna mashtaka yoyote yaliyowasilishwa dhidi yake.
Watetezi wa masuala ya utawala bora wameipongeza hatua hiyo kama jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
"Hili ni jambo la kimaadili na kiutekelezaji kuwahi kutangazwa na rais wa Ghana aliye madarakani," Emmanuel Wilson Jr, mwanaharakati wa kupinga ufisadi wa shirika la ‘Crusaders Against Corruption’, ameiambia AFP.
Katika hotuba yake, Mahama aliahidi kuwa onyo hilo "si la mzaha. litatekelezwa. Na sitosita kuchukua hatua kali na madhubuti, bila kujali nani anahusika."
Marufuku kuhusu zawadi
Vifungu muhimu vya kanuni hiyo ni kuweka wazi mali mtu anazomiliki, kuzingatia mgongano wa kimaslahi, wateule kununua mali za serikali, marufuku kuhusu kupokea zawadi ya thamani zaidi ya GHS20,000 ($1,500) na utaratibu mkali wa kuidhinisha safari za kiserikali.
Kutakuwa na mtandao maalum ili kutoa nafasi kwa raia kutoa taarifa kwa siri kwa wale wanaokiuka kanuni hiyo ya maadili.
Ufisadi ulikumba serikali ya rais wa zamani Nana Akufo-Addo, na kusababisha uchumi wa Ghana kuyumba na kujikuta katika hali waliyoko sasa.
Comments
No comments Yet
Comment