Dollar

38,5591

-0.03 %

Euro

43,6267

-0.04 %

Gram Gold

4.112,8900

2.34 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

‘Tunashkuru serikali ya Marekani kwa operesheni hii ya usalama iliyofanikiwa,’ alisema waziri wa mambo ya ndani

Walanguzi kadhaa wa dawa za kulevya wakamatwa Malawi

Serikali ya Malawi, kwa ushirikiano na maafisa wa Marekani wamefanya operesheni ya usalama, na kufanikiwa kuwakamata walanguzi saba wa dawa za kulevya wenye uhusiano na magenge ya nchini Mexico, waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo alisema Jumatatu.

Washukiwa sita wamekamatwa walipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu kwenye mji mkuu Lilongwe waliposhuka kutoka katika ndege ya shirika la Ethiopia, Waziri wa Mambo ya ndani Ezekiel Ching’oma ameliambia shirika la habari la Anadolu.

Mshukiwa wa saba, raia wa Nigeria anayeishi Lilongwe, alikamatwa wakati akisubiri hao wenzake sita.

Njia ya kupitisha mihadarati

“Tumebaini kuwa walanguzi hawa wana uhusiano na magenge ya dawa za kulevya ya Mexico. Lakini uchunguzi bado unaendelea kupata taarifa zaidi. Tunaishkuru sana serikali ya Marekani kwa mafanikio ya operesheni hii ya usalama,” aliongeza.

Kulingana na shirika la ENACT, linalofuatilia masuala ya uhalifu barani Afrika, Malawi sasa imekuwa njia inayopendelewa na walanguzi wa mihadarati.

Njia ya nchi hiyo unafahamika zaidi kwa kupitisha dawa za heroin kutoka Afrika Mashariki hadi Kusini mwa Afrika na Eswatini.

Hata hivyo, pia nchi hiyo inatumika kama njia ya dawa zingine za kulevya, ikiwemo cocaine, inayovushwa kutoka Msumbiji hadi bara Ulaya au Asia kwa njia ya ndege, shirika hilo lilieleza.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#