Dollar

38,5864

0.04 %

Euro

43,7785

0.32 %

Gram Gold

4.114,9300

2.39 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kikosi cha Rapid Support Forces, RSF kinachovutana na jeshi la Sudan, kilifanya shambulio la ndege isiyo na rubani Jumapili, kwenye kambi ya jeshi la anga na vituo vyengine karibu na Uwanja wa Ndege wa Port Sudan.

Umoja wa Afrika walaani mashambulizi ya Port Sudan

Umoja wa Afrika, AU, umeoyesha wasiwasi mkubwa kwa shambulio la hivi majuzi la Port Sudan, mji wa kimkakati ambao umesalia kuwa moja ya maeneo machache tulivu katika Jamhuri ya Sudan huku kukiwa na mzozo unaoendelea.

Kikosi cha RSF kinachovutana na jeshi la Sudan, kilifanya shambulio la ndege isiyo na rubani Jumapili, kwenye kambi ya jeshi la anga na vituo vyengine karibu na Uwanja wa Ndege wa Port Sudan.

“Umoja wa Afrika unalaani vikali shambulio hili, ambalo linawakilisha ongezeko la hatari katika mzozo unaoendelea na tishio la moja kwa moja kwa maisha ya raia, ufikiaji wa misaada ya kibinadamu, na utulivu wa kikanda,” Umoja wa Afrika umesema katika taarifa.

RSF haijatoa maoni yoyote kuhusu tukio hilo. Wakati huo huo, jeshi la Sudan limesema kuwa limetungua ndege zisizo na rubani zilizolenga kituo cha anga cha Osman Digna na miundombinu ya kiraia katika mji wa mashariki wa Port Sudan.

Umoja wa Afrika umesisitiza dhamira yake thabiti ya ulinzi kwa raia, na kukemea vikali vitendo vyote vinavyodhoofisha juhudi za amani, kutatiza shughuli za kibinadamu, au kulenga miundombinu muhimu.

“Port Sudan imekuwa na jukumu muhimu kama kitovu cha vifaa na kibinadamu wakati wa mzozo wa sasa. Mashambulizi yoyote yanayoilenga sio tu tishio kwa usalama wa watu wasio na hatia bali pia hudhoofisha juhudi zinazoendelea za kuleta utulivu nchini,” AU imesema.

Umoja wa Afrika umesema utatumia Jopo lake la Ngazi ya Juu, wataalamu walioteuliwa kufuatilia amani nchini sudan, ambayo unasema unaendelea kujishughulisha kikamilifu katika juhudi za kuwezesha mazungumzo, upatanishi kati ya pande zote, na kuunga mkono mipango ya amani ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Umoja wa Afrika unatoa wito kwa wadau wote kuunga mkono upatanishi unaoongozwa na Afrika na kuweka maslahi ya watu wa Sudan juu ya yote.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#