Dollar

38,5842

0.04 %

Euro

43,8036

0.37 %

Gram Gold

4.112,0900

2.32 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Waasi wa M23 na washirika wake wachukua udhibiti wa mji wa Lunyasenge magharibi mwa pwani ya Ziwa Edward kaskazini mwa DRC.

M23 yadhibiti mji wa kimkakati wa wavuvi mashariki mwa DRC licha ya makubaliano ya amani

Waasi wa M23 na washirika wake Jumapili wameuchukua mji wa Lunyasenge magharibi mwa pwani ya Ziwa Edward kaskazini mwa DRC, kufuatia mapigano na jeshi ambayo yalisababisha vifo vya watu 17, ikiwemo wanajeshi saba.

Jeshi la Congo limethibitisha katika taarifa yake kwamba Lunyasenge imechukuliwa katika mkoa wa mashariki ya Kaskazini mwa Kivu.

Kanali Mak Hazukay, msemaji wa jeshi wa eneo la Kaskazini, amelaani shambulio hilo na kuliita, “uvunjifu wa makusudi wa makubaliano ya kusitisha mapigano huku hatua zote zikiwa zimechukuliwa kufuatia majadiliano yanayoendelea Doha, Qatar, na Washington, Marekani.”

Hazukay amesema, jeshi la Congo lina “haki ya kujibu kwa njia yoyote iwapo kutaendelea kuwa na tishio kutoka kwa waasi na washirika wao wa Rwanda.”

Eneo la kimkakati la uvuvi

Msemaji katika taarifa iliyotolewa, haikutaja mapigano au vifo, lakini afisa mmoja kutoka eneo hilo, ameiambia Anadolu kwa njia ya simu, bila kutaka kutajwa jina lake, kwa sababu hakuwa na mamlaka ya kuongea na vyombo vya habari, kwamba, wanajeshi saba na waasi kumi wameuawa katika mapigano.

Kwa upande wake, wakazi wa eneo hilo wanadai kwamba waasi wamekuja katika fukwe wakitokea eneo la uvuvi la Vutsumbi na Kamandi.

“Nimeshuhudia mwenyewe, baadhi yao wamevuka ziwa na kuingia nchi kavu,” Muhisa Ngeloko, mkazi ameiambia Anadolu, akithibitisha kwamba waasi wamepigana na wanajeshi wa Congo katika mji wa Lunyasenge.

Lunyasenge ni mji wa kimkakati wa wavuvi uliopo takriban mwendo wa saa nne kwa boti kutoka Kyavinyonge, eneo muhimu pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Virunga, iliyopo kaskazini mwa pwani ya Ziwa Edward.

Mazungumzo ya amani ya DRC, Rwanda

Kundi la M23 likiwa katikati ya mgogoro mashariki mwa DR Congo, limezidisha mapambano tangu mwezi Disemba, huku likishika miji muhimu ikiwemo Goma na Bukavu.

Kinshasa na wengine wamekuwa wakiilaumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuunga mkono M23, tuhuma ambazo Kigali imekuwa ikizikana.

Mwezi Machi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikubaliana kusitisha mapigano katika mazungumzo yaliyofanyika Doha na kusimamiwa na Emir wa Qatar.

Licha ya makubaliano hayo, mapigano yamekua yakiendelea katika maeneo ya Kaskazini mwa mkoa wa Kivu.

Kuheshimu mipaka

Mwezi Aprili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo Therese Kayikwamba Wagner na mwenzake wa Rwanda Olivier Nduhungirehe walitia saini makubalino yaliyosimamiwa na Marekani mjini Washington.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alihudhuria tukio hilo.

Pande zote mbili ziliahidi kuheshimu mipaka ya nchi zao na kuandaa makubaliano ya amani kufika Mei 2 kumaliza uhasama uliopo mashariki mwa DR Congo, lakini mpaka sasa hakuna taarifa iliyotolewa kuhusiana na makubaliano hayo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#