Sport
Dollar
38,5929
0.02 %Euro
43,7562
0.02 %Gram Gold
4.133,7100
-0.01 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imetupilia mbali kesi ya Sudan dhidi ya UAE ya madai ya kuhusika katika mauaji ya halaiki kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan.
Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu ilitupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Sudan dhidi ya UAE kwa madai ya kuhusika na mauaji ya halaiki wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.
Sudan iliwasilisha kesi katika mahakama ya ICJ, ikidai kuwa kuwaunga mkono wapiganaji wa RSF kunachangia mauaji ya halaiki – madai ambayo UAE imekanusha.
Lakini ICJ imesema "ni wazi haina" mamlaka ya kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo na ikaitupilia mbali.
Wakati UAE ilipotia saini makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya halaiki 2005, iliweka wazi kuhusu "wasiwasi wake" wa kifungu cha nchi kushitakiana ICJ kufuatia migogoro.
'Hayana msingi'
Kwa wasiwasi wake huu kulimaanisha ICJ haikuwa na mamlaka ya kujihusisha na kesi hiyo.
Afisa mmoja wa UAE ameusifu uamuzi huo wa majaji.
"Uamuzi huu ni uthibitisho wa wazi kuwa kesi hii haina msingi wowote," Reem Ketait, Naibu Waziri wa Masuala ya Siasa katika wizara ya mambo ya nje ya UAE, alisema katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.
Kabla ya uamuzi huo, Ketait aliishtumu Sudan kwa kuwasilisha kesi "yenye lengo la kutatiza watu wasiangazie mauaji ya kikatili wanaofanya wao dhidi ya raia wa Sudan."
Kung’ang’ania madaraka
Tangu Aprili 2023, Sudan imekumbwa na vita kutokana na mapigano ya kugombania madaraka kati ya kiongozi wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na kamanda wa wapiganaji wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo.
Vita hivi vimesababisha kile mashirika ya misaada ilichokitaja kuwa hali mbaya zaidi kwa watu duniani na njaa kali. Sasa hivi ni rasmi, kuna njaa kali katika maeneo matano kote Sudan,kulingana na tathmini inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Eneo la Darfur Kaskazini limekuwa sehemu ya mapigano,huku raia wasiopungua 542 wakiwa wameuawa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, kulingana na Umoja wa Mataifa.
ICJ inasema "ina wasiwasi mkubwa kuhusu majanga yanayoibuka kwa watu wa Sudan ambayo chanzo chake ni mvutano unaoendelea sasa."
'Athari mbaya'
"Mapigano yamekuwa na athari mbaya, iliyosababisha watu kupoteza maisha na mateso, hasa Magharibi mwa Darfur," mahakama iliongeza.
Na huku mahakama ikisema kuwa haina mamlaka ya kuendelea na kesi ya Sudan, haikutoa hukumu kuhusu masuala ya msingi ya kesi yenyewe.
Mahakama imeamua hivi: "Iwapo taifa limekubali au limekataa mamlaka ya mahakama... wanatakiwa kutekeleza jukumu lao kuhusu (Makubaliano kuhusu Mauaji ya halaiki)."
Nchi pia "zinakuwa na jukumu kuhusu madai wanayonasibishwa nayo ambayo ni kinyume na matarajio ya kimataifa".
Waandamanaji wanaounga mkono Sudan
Waandamanaji wachache wanaounga mkono Sudan waliandamana nje ya mahakama ya ICJ mjini The Hague, wakieleza yanayowakwaza na kubeba mabango ikiwemo moja lililosomeka "UAE inaua Sudan."
"Tumevunjika moyo sana .... tunataka haki tu," alisema mmoja wa waandamanaji, Hisham Fadl Akasha, mhandisi mwenye umri wa miaka 57.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo mwezi uliopita, Kaimu waziri wa sheria wa Sudan Muawia Osman aliiambia mahakama kuwa "mauaji ya halaiki yanayoendelea kwa sasa yasingewezekana bila msaada wa UAE, ikiwemo kuwapelekea silaha RSF."
"Msaada ambao UAE umewapa na inaendelea kuwapa RSF na unachochea mauaji ya halaiki, ikiwemo mauaji, ubakaji, kuwaondoa watu kwa lazima kutoka maeneo yao na uporaji," alisema Osman.
Fidia
Sudan ilitaka majaji wa ICJ kuwashurutisha UAE kusitisha msaada unaodaiwa kwa RSF na "kutoa fidia kamili", ikiwemo kuwalipa wale walioathirika na vita.
Wakati ICJ ikikataa kesi ya Sudan, mapigano nchini Sudan hayaoneshi dalili ya kusitishwa.
Siku ya Jumapili, wapiganaji wa RSF walishambulia mji wa Port Sudan, jeshi limesema, ikiwa ni shambulio la kwanza kulenga yaliokuwa makao makuu ya jeshi wakati wa vita vya miaka miwili vya nchi hiyo.
Comments
No comments Yet
Comment