Dollar

38,7786

0.39 %

Euro

43,8944

0.27 %

Gram Gold

4.147,5900

1.06 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kuondoka Chadema kwa viongozi hawa, kunakuja siku kadhaa, za kujiondoa kwa kundi jengine la viongozi wa chama hicho kikongwe cha upinzani Tanzania, hivyo kuibua wasiwasi miongoni mwa wananchi na wadau wa kisiasa kuhusu hatma ya chama hicho

Viongozi zaidi wajivua uanachama Chadema, kunani?

Chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kinaonekana kupitia wakati mgumu baada ya viongozi wake kadhaa kutoka kanda nane upande wa Tanzania Bara kujivua uanachama Mei 10, 2025.

Viongozi hao ni kutoka kanda ya Pwani, Kaskazini,  Serengeti, Kusini, Kati, Nyasa, Victoria na Magharibi.

Katika taarifa yao ya pamoja, viongozi hao, wamedai kuwa hatua hiyo inafuatia kukithiri kwa ukiukwaji wa Katiba ya Chama, pamoja na kukithiri kwa chuki na ubaguzi dhidi ya viongozi na makada waliokuwa wakimuunga mkono aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe.

“Uamuzi wa Chama kutoshiriki uchaguzi na hivyo kuiacha CCM ipite bila upinzani madhubuti,” imetaja taarifa hiyo kama moja ya sababu ya viongozi hao kuondoka Chadema.

Miongoni mwa waliotangaza kujivua uanachama ni Jackson Jingu – aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Kanda ya Kati, Emma Kimambo – aliyekuwa Mweka Hazina Kanda ya Kaskazini, Basil Lema – aliyekuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro.

Pia yuko Gimbi Masaba – aliyekuwa Makamu Mwenyekiti BAWACHA Kanda ya Serengeti na aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa na Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Esther Fulano – aliyekuwa Katibu wa BAWACHA Kanda ya Victoria na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema Taifa.

Wengine ni Doris Mpatili – aliyekuwa Mwenyekiti Kamati ya Mafunzo Kanda ya Victoria, Hadija Said Mwago – aliyekuwa  Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema kupitia BAWACHA, Mwenyekiti wa BAWACHA Jimbo la Mbagala na Mgombea Ubunge wa CHADEMA Jimbo la Mbagala 2020 na wengine kadhaa.

Kujiondoka Chadema kwa viongozi hawa, kunakuja siku kadhaa, baada ya kujiondoa kwa kundi jengine la viongozi wa chama hicho kikongwe cha upinzani Tanzania, hivyo kuibua wasiwasi miongoni mwa wananchi na wadau wa siasa kuhusu hatma ya chama hicho na mwelekeo wa upinzani kwa ujumla.

Wakati hayo yanajiri, kiongozi mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambae ni Mwenyekiti Taifa anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo la uhaini ambalo kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo, halina dhamana.

Hata hivyo, kukamatwa kwake, kumeibua hisia tofauti, ikiwemo Bunge la Ulaya ambalo, limeitaka serikali kumwachilia mara moja kiongozi huyo.

Hatua ambayo, serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imesema kuwa Bunge hilo la Ulaya halina haki ya kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania ikiwemo mahakama.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#