Sport
Dollar
38,7786
0.39 %Euro
43,8944
0.27 %Gram Gold
4.147,5900
1.06 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, alikamatwa nchini Cameroon tangu Januari alipokuwa akijaribu kupanda ndege na kuelekea nchini Ufaransa.
Kiongozi wa waasi Armel Sayo, ambae alikuwa anatafutwa kuhusiana na mashambulizi dhidi ya jeshi, alikamatwa nchini Cameroon kabla ya kupelekwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, maafisa wamesema.
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inamshikilia kiongozi wa waasi na aliyekuwa waziri ambae ameshtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, mwendesha mashtaka amesema siku ya Ijumaa.
Armel Sayo, ambae alikuwa anatafutwa kuhusiana na mashambulizi kadhaa dhidi ya jesh, alikamatwa nchini Cameroon na kurudishwa Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu siku ya Jumatatu, imesema ofisi ya mwendesha mashtaka katika taarifa yake.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, alikamatwa Cameroon tangu Januari alipokuwa anajaribu kupanda ndege na kuelekea Ufaransa.
Sayo, mwenye umri wa miaka 45, ni kiongozi wa kundi la wapiganaji la CMSPR. Na pia amewahi kuwa waziri katika serikali zilizopita.
Washirika washikiliwa
Waendesha mashtaka wamesema, washirika wa Sayo pia wameshikiliwa. Nchi hiyo imekubwa na vurugu za mara kwa mara tangu uhuru mwaka 1960.
Comments
No comments Yet
Comment