Sport
Dollar
38,7409
-0.06 %Euro
43,5340
-0.26 %Gram Gold
4.084,2200
-1.43 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mvua ya mwishoni mwa juma iliyonyesha kwa takriban saa nane, imeleta mafuriko na uharibifu mkubwa wa miundombinu.
Takriban watu saba wamepoteza maisha huku miundombinu ya barabara kubwa ikiharibiwa baada ya mvua kubwa kunyesha katika mji mkuu wa Mogadishu, nchini Somalia.
Mvua hiyo iliyonyesha siku ya Ijumaa ilisababisha mafuriko baada ya miundombinu ya maji taka kuzidiwa.
Mafuriko yaliharibu miundombinu muhimu, na kuathiri usafiri wa umma, ikiwemo kusimamisha kwa muda mfupi huduma za uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Aden Abdulle.
Maafisa baadae walithibitisha ndege kuanza kuruka.
Msemaji wa eneo hilo, Abdinasir Hirsi Idle, ameliambia Shirika la Associated Press Jumamosi kwamba jitihada za uokozi zinaendelea.
Saa nane za mvua
“Idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa sababu mvua zilikuwa kubwa na za muda mrefu, hivyo kusababisha nyumba tisa kuanguka katika maeneo jirani, na takriban barabara sita kubwa kuharibiwa vibaya,” amesema.
Mvua za Ijumaa zilinyesha kwa takriban saa nane, na maji kufikia usawa wa kiuno katika maeneo jirani ambapo baadhi ya wakazi hawakuwezi kutoka, huku wengine wakilazimika kwenda maeneo yenye mwinuko.
Somalia imekuwa ikikabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ni pamoja na kiangazi kikali na kirefu kilichosababisha ukame na wakati mwengine mvua kubwa zinazosababisha mafuriko.
Mohamed Hassan ambae ni mkazi ameiambia AP kwamba baadhi ya wazee hawakuweza kutoka katika maeneo yao.
“Tulikuwa juu ya mapaa usiku kucha, tukitetemeka kwa baridi, na pia sijapata kifungua kinywa,” amesema.
Kiwango cha hasara
Ofisi ya Wakala wa Kushughulikia Majanga nchini Somalia bado haijatola idadi kamili ya vifo lakini imesema tathmini inaendelea kubaini kiwango cha uharibifu.
Kwa upande wake, wizara ya maji na nishati imesema katika taarifa yake ya Jumamosi, “mvua kubwa, inayozidi milimita 115, imerikodiwa kwa saa nane mfululizo” na kutahadhirisha mafuriko katika mikoa mengine nje ya mji mkuu.
Comments
No comments Yet
Comment