Dollar

38,7659

0.01 %

Euro

43,1338

-1.23 %

Gram Gold

4.038,7500

-2.53 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Waziri wa Afya wa jimbo la Kivu Kusini Theophile Walulika Muzaliwa amewaambia waandishi wa habari kuwa juhudi za utafutaji na uokoaji zimetatizwa pakubwa.

Mafuriko yasababisha vifo zaidi DRC

Zaidi ya watu 100 wameripotiwa kufa baada ya mafuriko katika kijiji cha karibu na mwambao wa Ziwa Tanganyika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hayo ni kwa mujibu wa afisa wa eneo hilo.

Waziri wa Afya wa jimbo la Kivu Kusini Theophile Walulika Muzaliwa amewaambia waandishi wa habari kwamba juhudi za utafutaji na uokoaji zimetatizwa pakubwa.

"Machifu wa sekta, machifu wa vijiji na machifu wa mitaa, ambao pia ni wajumbe wa serikali ya mtaa, wapo kwenye eneo hilo. Shirika pekee la kibinadamu lililopo kwa sasa ni la Msalaba Mwekundu. Haiwezekani kutoa tathmini kwa kuwa upekuzi wa miili unaendelea," alisema Muzaliwa.

Mafuriko hayo yaliyoathiri kijiji cha Kasaba yanakuja wakati ambapo waasi wa M23 wameshambulia sehemu za Kivu kaskazini na tayari kusababisha maelefu kuhama makazi yao.

Waasi wa M23 wamezidisha mashambulizi katika eneo la mashariki tangu kuanza kwa mwaka huu, huku maelfu wakiuawa katika mapigano katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka.

Samy Kalodji, ambae ni msimamizi wa eneo la Fizi katika jimbo la Kivu Kusini ambako kijiji hicho kinapatikana, alisema Jumamosi kwamba ripoti kutoka eneo hilo "zilionyesha zaidi ya vifo 100."

Eneo lililoathiriwa bado liko chini ya usimamizi wa Kinshasa na si miongoni mwa kanda zilizochukuliwa na M23.

Didier Luganywa, msemaji wa serikali ya Kivu Kusini, alisema katika taarifa yake kuwa tukio la mafuriko lilitokea kati ya Alhamisi usiku na Ijumaa wakati mvua kubwa na upepo mkali na kusababisha mto Kasaba kufurika kingo zake.

Mafuriko hayo yametokea wiki kadhaa baada ya mvua kama hiyo kuwauwa waathiriwa 33 katika mji mkuu wa Kinshasa. Miundombinu kote nchini imeathiriwa katika miezi ya hivi karibuni, huku mwitikio wa kibinadamu ukiwa na mzozo katika eneo hilo.

Maeneo mengine yaliyoathiriwa na mvua kubwa mwishoni mwa juma ni Somalia, ambapo mvua kubwa ziliharibu miundombinu ya mji mkuu wa Mogadishu na kuharibu barabara sita kuu za mji huo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#