Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kunufaika na ushirikiano wa kimkakati na Marekani katika utafiti, uwekezaji katika sekta ya madini, hususan madini yanayohitajika kwa wingi katika teknolojia za kisasa duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alisema ushirikiano huo utawezesha kufanyika kwa utafiti wa kina katika baadhi ya leseni zinazomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kwa lengo la kubaini maeneo yenye fursa kubwa za uwekezaji.
Utafiti huo unatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ambayo ina viashiria vikubwa vya uwepo wa madini ya kinye (graphite), madini muhimu katika utengenezaji wa betri za magari ya umeme, nishati mbadala na teknolojia za kisasa.
Waziri Mavunde alisema mahitaji ya graphite duniani yanakadiriwa kufikia tani milioni 4.5 kwa mwaka ifikapo 2050, hali inayoiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kuwa miongoni mwa wasambazaji wakuu wa madini hayo duniani.
Mbali na utafiti, ushirikiano huo pia unalenga kuwajengea uwezo wataalamu wa Tanzania kupitia mafunzo ya teknolojia za kisasa za utafiti wa madini.
Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, alisema Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta ya madini ili kuongeza thamani ya rasilimali, kuvutia uwekezaji na kuchangia ukuaji wa uchumi endelevu.
Ushirikiano huo unaelezwa kuwa sehemu ya jitihada za pamoja za kuimarisha maendeleo ya sekta ya madini kwa manufaa ya pande zote.
Comments
No comments Yet
Comment