Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kulingana na orodha hiyo ya ubora ya FIFA, Tanzania imevuna jumla ya alama 1186.14 kutoka alama 1181.22, ilizokuwa nazo awali.

Tanzania yapanda juu nafasi mbili viwango vya ubora wa soka vya FIFA

Timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, imepanda kwa nafasi mbili kwenye orodha ya viwango vya ubora wa soka duniani, iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa Duniani (FIFA), Januari 19, 2026.

‘Taifa Stars’, ambayo ilifanikiwa kuingia hatua ya mtoano ya michuano ya AFCON 2025, iliyomalizika hivi karibuni nchini Morocco, imekwea juu kwa nafasi mbili, kutoka ile ya 112 hadi 110, kufuatia mafanikio yake kwenye michuano hiyo ambayo ilishuhudia Senegal ikitawazwa kuwa mabingwa kwa mara ya pili, katika historia yao.

Kulingana na orodha hiyo ya ubora ya FIFA, Tanzania imevuna jumla ya alama 1186.14 kutoka alama 1181.22.

Wakati huo huo, mabingwa wa Afrika, Senegal, wamekwea hadi nafasi ya 12 duniani kutoka ile ya awali ya 19, kufuatia mafanikio yao kwenye michuano ya AFCON 2025.

‘Simba wa Teranga’ wameibuka vinara, wakiipiku Italia, Colombia na Marekani, kwa mujibu wa orodha hiyo ya FIFA.

Kwa upande wao, Morocco ambao waliishia kwenye hatua ya fainali, wamepanda hadi nafasi ya 8 duniani, wakiyapiku mataifa mengine kama Ujerumani, Ubelgiji na Ugiriki.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#