Dollar

43,2855

0.06 %

Euro

50,8066

0.78 %

Gram Gold

6.589,7600

1.44 %

Quarter Gold

10.936,4100

1.61 %

Silver

130,4100

-0.64 %

Huu utakuwa mkutano wa kwanza wa viongozi hao wawili.

Sisi wa Misri kukutana na Trump Davos

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump pembeni mwa Kongamano la Kiuchumi la Dunia mjini Davos, ofisi ya rais wa Misri ilisema Jumanne.

Huu utakuwa mkutano wa kwanza wa viongozi hawa wawili tangu Marekani itangaze kuanza kwa mpango wake wa kumaliza vita vya Gaza.

Sisi na Trump walikutana katika mji wa kitalii wa Sharm el-Sheikh mwezi Oktoba wakati wa mkutano ulioitishwa na Misri kusaini makubaliano ya kusitisha vita.

Siku ya Ijumaa, Trump alisema kuwa yuko tayari kuanzisha tena mchakato wa upatanishi wa Marekani kati ya Misri na Ethiopia kutatua mzozo wa bwawa la Ethiopia, ambalo mataifa ya Misri na Sudan yanaliona kama tishio kwa usambazaji wao wa maji.

Kutibuka kwa mazungumzo

Upatanishi unaoratibiwa na Marekani ulianza katika muhula wa kwanza wa Trump, lakini ulitibuka 2020, wakati Ethiopia ilipojiondoa — ingawa sehemu ya majadiliano baadaye iliendelea chini ya Umoja wa Afrika.

Ethiopia ilizindua rasmi Bwawa hilo, mwaka uliopita. Ikiwa bwana kubwa zaidi barani Afrika, liko katika eneo la Blue Nile karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan na linatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 5,000, kuongeza maradufu uwezo wa Ethiopia wa kuzalisha umeme.

Ethiopia inaona bwawa hilo litaimarisha uchumi wao. Lakini Misri ilipinga kujengwa kwake, ikidai kuwa litapunguza sehemu yake ya maji ya Mto Nile, ambayo inategemea kwa sehemu kubwa kwa kilimo na kusambaza maji kwa raia wake zaidi ya milioni 100.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#