Dollar

43,2914

0.07 %

Euro

50,8113

0.79 %

Gram Gold

6.574,9600

1.21 %

Quarter Gold

10.889,7000

1.18 %

Silver

132,3800

0.86 %

“Ushahidi unaonyesha kuwa matukio ya ukatili iliyoshuhudiwa El Geneina mwaka 2023 yamerudiwa Al Fasher mwaka 2025,” anasema naibu mwendesha mashtaka Nazhat Shameem Khan.

ICC yapata ushahidi wa uhalifu wa kivita nchini Sudan

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imesema imepata ushahidi unaoonyesha kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu umefanywa katika eneo la Darfur nchini Sudan, ikitaja ukatili unaojirudia katika mji wa Al Fasher na matumizi ya ukatili wa kingono kama silaha ya vita.

Naibu mwendesha mashtaka wa ICC, Nazhat Shameem Khan, aliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa tathmini ya ofisi yake ilitokana na data ya video, sauti na picha za satelaiti zilizokusanywa katika kipindi cha utoaji wa ripoti.

“Kwa kuzingatia taarifa na ushahidi uliokusanywa na ofisi katika kipindi hiki cha kuripoti, ikiwemo video, sauti na data za satelaiti, tathmini ya ofisi ya mwendesha mashtaka ni kwamba uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu umefanywa Al Fasher, ikiwemo mwezi wa Oktoba wakati wa kuzingirwa kwa mji huo na wanamgambo wa RSF,” alisema.

Khan alisema kuwa nyenzo za video zinaonyesha “mfumo unaofanana wa uhalifu uliowahi kuonekana hapo awali, unaodaiwa kutekelezwa na RSF katika maeneo mengine ya Darfur, ikiwemo kuwazuilia, kuwatesa na kuwaua watu kutoka makabila yasiyo ya Kiarabu.”

‘Ukatili unaojirudia’

“Ushahidi unaonyesha kuwa mifumo ya ukatili iliyotokea El Geneina mwaka 2023 imerudiwa Al Fasher mwaka 2025. Uhalifu huu unarudiwa katika miji ya Darfur,” alisema, akiongeza: “Ni jambo lisilopingika, kwa mujibu wa uchunguzi wetu, kwamba ukatili wa kingono, ikiwemo ubakaji, unatumika kama silaha ya vita huko Darfur.”

Khan alitaja hukumu ya mwezi Oktoba 2025 dhidi ya Ali Mohammed Abdul Rahman kama hatua muhimu, akiita “hukumu ya kwanza iliyotokana na rufaa ya Baraza la Usalama kwa mahakama,” na pia ya kwanza kwa misingi ya mateso yanayohusishwa na unyanyasaji wa kijinsia.

Alisema uchunguzi unakabiliwa na changamo kutokana na ufikiaji mdogo wa maeneo na usalama wa mashahidi, lakini alibainisha kuwepo kwa ushirikiano ulioboreshwa na nchi za Afrika na mamlaka za Sudan, ikiwemo misheni zilizoko Port Sudan.

“Uchunguzi wa kina, wa kimfumo na wenye ufanisi kwa uhalifu huu utaendelea kuwa kipaumbele kikuu katika kipindi kijacho,” aliongeza.

Marekani yamnyima Khan visa

Kabla ya kulihutubia Baraza, Khan alianza kwa kueleza “masikitiko” yake kwa kutoweza kuwasilisha kazi ya mahakama kuhusu Sudan ana kwa ana kutokana na kunyimwa visa na Marekani.

“Nasikitika kwamba sikupata visa ili niweze kutoa taarifa yangu kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na Baraza,” alisema.

Kwa mujibu wa Mkataba wa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, nchi mwenyeji—katika suala hili ambalo ni Marekani—inalazimika kutoa visa kwa watu wanaotekeleza shughuli rasmi za Umoja wa Mataifa, bila kujali uhusiano wa kidiplomasia.

Wanachama wengi wa Baraza walieleza kumuunga mkono Khan na kuonyesha masikitiko yao kwa kunyimwa kwake visa.

Tishio la kuchukuliwa kwa hatua zaidi

Hata hivyo, naibu mjumbe wa Marekani, Jeff Bartos, alitishia kuchukua hatua zaidi dhidi ya ICC na kusema: “Ingawa mgogoro wa Sudan ni suala linalostahili kuangaliwa na Baraza hili, inasikitisha kwamba naibu mwendesha mashtaka wa ICC—ambaye Marekani imemwekea vikwazo kwa kuunga mkono hatua zisizo halali za ICC—alialikwa kutoa taarifa leo.”

“Marekani inaendelea kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu jitihada za ICC kudai mamlaka juu ya Marekani au mshirika yeyote wa Marekani ambaye hajakubali mamlaka ya ICC,” alisema, akiongeza: “Hatutavumilia mahakama inayojaribu kudhoofisha mamlaka ya Marekani, na tumekuwa tukichukua hatua stahiki kulinda maslahi yetu.”

Alisisitiza kuwa “mwitikio wa Marekani utaendelea kuongezeka kulingana na kiwango cha tishio kinachowasilishwa na kwa kiwango ambacho wasiwasi wetu wa muda mrefu bado haujashughulikiwa.”

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#