Sport
Dollar
43,2894
0.06 %Euro
50,7680
0.69 %Gram Gold
6.580,6800
1.3 %Quarter Gold
10.857,6800
0.88 %Silver
132,7700
1.16 %Kwa sasa, sehemu kubwa ya Msumbiji imemezwa na mafuriko, hatua iliyopelekea kiongozi wa nchi hiyo, Daniel Chapo kuahirisha safari yake ya kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi utakaofanyika jijini Davos, Uswisi.
Taifa la Msumbiji linaendelea kukabiliana na hali mbaya ya mafuriko, huku idadi ya vifo iikizidi kuongezeka.
Taarifa zinaonesha kuwa, Msumbiji pamoja na Afrika Kusini zimekumbwa na mafuriko kwa wiki kadhaa sasa, huku watu wapatao 150 wakiripotiwa kupoteza maisha.
Kwa sasa, sehemu kubwa ya Msumbiji imemezwa na mafuriko, hatua iliyopelekea kiongozi wa nchi hiyo, Daniel Chapo kuahirisha safari yake ya kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi utakaofanyika jijini Davos, Uswisi.
Wakati huo huo, idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko hayo, imefikia 37, katika maeneo ya kaskazini magharibi mwa Limpopo na Mpumalanga, mpakani mwa Msumbiji na Afrika Kusini.
Kingo za mito zinaripotiwa kubomoka nchini Msumbiji, hali iliyosababisha maeneo mengi kusombwa na maji, na kuwaacha watu wengi bila makazi, akiwemo mwanamke mmoja aliyejifungua juu la paa la nyumba.
Comments
No comments Yet
Comment