Dollar

43,2887

0.06 %

Euro

50,7771

0.71 %

Gram Gold

6.578,4700

1.26 %

Quarter Gold

10.854,1200

0.85 %

Silver

132,4800

0.94 %

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imenukuu vyanzo vya serikali vikikadiria kuathirika kwa zaidi ya watu 400,000

Rais Chapo avunja safari ya Davos kwa sababu ya mafuriko Msumbiji

Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo, ameghairisha safari yake ya kwenda katika Mkutano wa Kiuchumi Duniani (World Economic Forum) huko Davos wiki hii kutokana na mafuriko makali ambayo yameharibu miundombinu na kuathiri mamia ya maelfu ya watu nchini humo.

Chapo aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook mwishoni mwa juma kwamba Msumbiji "inapitia wakati mgumu ... (na) kipaumbele kikuu kwa sasa ni kuokoa maisha."

Mvua kubwa zimekuwa zikiendelea tangu katikati mwa mwezi Disemba na kusababisha mafuriko katika mikoa ya Gaza, Maputo na Sofala ya Msumbiji, huku viwango vya mito kadhaa zikiwa juu, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilisema katika ripoti Jumapili.

Ripoti ya OCHA ilisema mamlaka zinakadiria kuwa watu zaidi ya 400,000 wameathiriwa, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka huku mvua zikiendelea.

Nchi jirani ya Afrika Kusini imetoa helikopta ya jeshi la anga kwenda Msumbiji kusaidia katika jitihada za utafutaji na uokoaji.

Mvua kubwa pia zimeathiri sehemu za Afrika Kusini, ikiwemo kaskazini-mashariki ambako kuna Hifadhi maarufu ya Taifa ya Kruger. Jumatatu, Kruger ilifunguliwa tena kwa watalii wa mchana baada ya kufungwa kwa siku kadhaa.

Mafuriko yamekuwa yakitokea mara nyingi zaidi na kwa kiwango kikubwa kusini-mashariki mwa Afrika, hii ikichangiwa na dhoruba zinazochangiwa na mabadiliko ya tabianchi katika Bahari ya Hindi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#