Sport
Dollar
43,3078
0.05 %Euro
50,7946
0.01 %Gram Gold
6.743,3800
1.89 %Quarter Gold
10.936,4100
0 %Silver
130,6700
-0.35 %Kulingana na Mashinda Mtei, ambaye ni mtoto wa Gavana huyo wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mzee Mtei anatarajiwa kupumzishwa katika kata ya Ambureni, eneo la Tengeru, Arusha, Jumamosi ya Januari 24.
Katibu Mkuu wa kwanza wa iliyokuwa Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki, Edwin Mtei anatarajiwa kuzikwa jijini Arusha nchini Tanzania, Jumamosi ya Januari 24, 2026.
Kulingana na Mashinda Mtei, ambaye ni mtoto wa tatu wa Mzee Mtei, Gavana huyo wa kwanza wa Benki kuu ya Tanzania (BOT), na Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), atazikwa katika kata ya Ambureni Eneo la Tengeru Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Akizungumzia kifo cha baba yake mapema Januari 20, Mashinda alisema Mzee Mtei amefariki kwa uzee, akiongeza kuwa, alishindwa hata kuzungumza kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kutokana na umri wake.
Mapema Januari 20, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Veronica Nduva, aliongoza wafanyakazi wa sekratariati ya Jumuiya hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha, kumkumbuka Mzee Mtei, ambaye ndiye Katibu Mkuu wa kwanza wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuvunjika mwaka 1977.
Mzee Mtei alihudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, kuanzia mwaka 1967 hadi 1971.

Katika kumbukumbu hiyo fupi, Nduva alimuelezea Mzee Mtei kama kiongozi hodari aliyeweka misingi ya ushirikiano wa kikanda na utangamano wa Afrika Mashariki, akiacha nyuma urithi ambao utaendelea kuongeza ushawishi mkubwa kwa vizazi vya Afrika Mashariki na kwingineko.
Mzee Mtei amefariki dunia usiku wa kuamkia Januari 20, akiwa na umri wa miaka 94.
Comments
No comments Yet
Comment