Dollar

43,3062

0.06 %

Euro

50,8424

0.16 %

Gram Gold

6.789,6000

2.59 %

Quarter Gold

11.290,5000

3.24 %

Silver

131,8400

0.55 %

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa “Syria iliyo na amani, isiyo na ugaidi na inayokua katika nyanja zote, itachangia utulivu wa eneo zima.”

Erdogan na Trump wamejadili hali ya Syria, Uturuki kuratibu na Marekani kuhusu Gaza

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, walifanya mazungumzo kwa njia ya simu kujadili uhusiano wa mataifa mawili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa, kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Rais Erdogan alimwambia Trump kuwa Uturuki inafuatilia kwa karibu yanayojiri nchini Syria, na kwamba umoja wa Syria, na uhuru wa mipaka yake ni mambo muhimu kwa Uturuki, taarifa hiyo ilisema siku ya Jumanne.

Viongozi hao pia walijadili kuhusu mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh na hali ya wanachama wa Daesh walioko katika magereza ya Syria.

Erdogan alisema kuwa “Syria iliyo na amani, isiyo na ugaidi na inayokua katika nyanja zote itachangia utulivu wa eneo hilo,” taarifa hio iliongeza.

Uturuki kuratibu na Marekani kwa ajili ya amani Gaza

Kuhusu Gaza, Erdogan alisema kuwa juhudi za kuanzisha amani Gaza zinaendelea, akiongeza kuwa Uturuki itaendelea kuchukua hatua kwa kuratibu na Marekani katika suala hilo.

Pia alimshukuru Trump kwa mwaliko wa kujiunga na Bodi ya Amani ya Gaza.

Mapema Jumanne, Trump alisema angefanya mazungumzo “muhimu sana” na Erdogan, “ambaye nampenda sana.”

Siku ya Ijumaa, Ikulu ya White House ilitangaza kuundwa kwa bodi hiyo ili “kuchukua nafasi muhimu katika kutekeleza” vipengele 20 vya mpango wa Trump wa kumaliza kabisa kile ilichokiita mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza na kuijenga upya Gaza, pamoja na “kutoa uangalizi wa kimkakati, kuhamasisha rasilimali za kimataifa, na kuhakikisha uwajibikaji Gaza inapobadilika kutoka kwenye mzozo kuelekea amani na maendeleo.”

Marekani pia iliunda Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Gaza kutekeleza awamu ya pili ya Mpango Kamili wa Trump wa Kumaliza Mgogoro wa Gaza, Bodi Kuu ya Utendaji ya waanzilishi, na Bodi ya Utendaji ya Gaza kusaidia mfumo wa mpito.

Trump amewaalika viongozi wengine wa nchi na serikali kujiunga na bodi hiyo, akiwemo Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#