Dollar

43,2819

0.22 %

Euro

50,2007

-0.1 %

Gram Gold

6.389,7100

-0.08 %

Quarter Gold

10.664,4800

0.75 %

Silver

124,1900

-2.76 %

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki anasema sera za Netanyahu, ambazo zimesababisha vifo na uharibifu katika eneo, zimeifanya Israel kutengwa kimataifa.

Hakuna anayetaka kupigwa picha na Netanyahu tena, anasema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amezidi kuifanya nchi yake kutengwa kwa kufuata sera kali za kijeshi ambazo zimesababisha vifo na uharibifu mkubwa katika eneo hilo, anasema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Istanbul siku ya Alhamisi, Fidan alisema kuwa katika mazingira ya sasa, kurejesha au kuhalalisha uhusiano na Israel limekuwa jambo lisilowezekana—sio tu kwa Uturuki, bali pia kwa nchi nyingi duniani.

“Kadiri hali hii inavyoendelea, kurejesha uhusiano na Israel ni jambo lisilowezekana si kwa Uturuki lakini kwa nchi nyingi ulimwenguni,” Fidan alisema, akiashiria operesheni za kijeshi zinazoendelea za Israel.

Kauli zake zilionyesha hali pana ya kidiplomasia ambapo uongozi wa Israel unakabiliwa na upinzani unaoongezeka, si tu kutoka kwa serikali, bali pia kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu na viongozi waliochaguliwa barani Ulaya.

Fidan aliangazia kutotaka kwa viongozi wa Ulaya kuonekana hadharani na Netanyahu, akibainisha kuwa wachache sana, au huenda hakuna kabisa, walio tayari kusafiri kwenda Israel au kupigwa picha wakiwa naye.

“Hakuna anayekwenda (Israel),” alisema. “Kwa nini hawaendi? Viongozi wa Ulaya wameingia madarakani kwa njia ya uchaguzi. Wanajua kuwa kupiga picha na Netenyahu si jambo zuri siku hizi.” 

Fidan alisema uwajibikaji wa kidemokrasia umekuwa sababu muhimu inayounda maamuzi ya sera za kigeni, huku viongozi wakipima mahusiano ya kidiplomasia dhidi ya matarajio na hisia za wapiga kura wao.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Uturuki alieleza msimamu huu ni ushahidi wa kuongezeka kwa kutengwa Israel kidiplomasia. Alihoji ikiwa Netanyahu anaweza kwa uhalisia kutembelea nchi yoyote nje ya Marekani, akidokeza kuwa hata washirika wa karibu wanazidi kuwa waangalifu.

“Je, anaweza kwenda popote nje ya Marekani? Hawezi. Labda atakuja Ugiriki,” Fidan alisema.

Fidan alisema kuwa msimamo wa Uturuki kuhusu Israel haupaswi kuonekana kama wa kipekee au unaoongozwa na itikadi fulani. Badala yake, aliuelezea kama sehemu ya mwitikio mpana unaoshirikiwa na jumuiya ya kimataifa.

“Huu si msimamo wetu peke yetu,” alisema. “Ni sera inayodhihirishwa na jumuiya ya kimataifa, inayoshiriki dhamira na maadili yale yale, kwa njia na mitindo tofauti.”

Fidan alisema baadhi ya nchi zimechagua kueleza waziwazi upinzani wao dhidi ya Israel, huku nyingine zikichagua njia za kimya za kujitenga, kwa kuepuka ziara za ngazi za juu na ishara za kimaandishi bila kutoa matamko ya hadharani.

Tofauti hii ya mitindo, alisema, haibadilishi kiini cha ujumbe unaotumwa kwa uongozi wa Israel.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#