Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Uturuki imeonya kuwa uingiliaji wowote wa nje katika nchi jirani ya Iran utaongeza na kuzidisha migogoro, si tu nchini humo bali pia katika eneo lote.

Uturuki yaonya dhidi ya uingiliaji wa nje nchini Iran, yatoa wito wa suluhu za ndani

Uturuiki imesisitiza kuwa matatizo ya ndani ya Iran yanapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo na mienendo ya kijamii ya taifa hilo lenyewe.

Msemaji wa Chama cha AK na Naibu Mwenyekiti wake, Omer Celik, alisema siku ya Jumatatu kuwa Uturuki haitamani kuona machafuko yakitokea Iran, licha ya kukiri kuwa kuna changamoto ndani ya jamii ya Iran na taasisi zake za serikali.

“Hatutamani kamwe kuona machafuko yoyote yakizuka kwa jirani yetu Iran,” Celik alisema katika mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho mjini Ankara, baada ya kikao kilichoongozwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Alisema kuwa, kama alivyobainisha Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, suluhu ya matatizo ya Iran inapaswa kupatikana kupitia suluhu za ndani za jamii ya Iran na dhamira ya kitaifa ya nchi hiyo.

Kuongezeka kwa machafuko

“Uingiliaji wa nje utasababisha madhara makubwa zaidi,” Celik alisema, akiongeza kuwa hasa uingiliaji unaochochewa na Israel unaweza kupelekea migogoro mikubwa na kuyumbisha zaidi utulivu wa eneo zima.

Akisisitiza kuwa suala hilo linapaswa kushughulikiwa kupitia mazungumzo, majadiliano na kuzidisha mawasiliano, Celik alisema kauli za hivi karibuni za maafisa wa Israel zinazolenga Iran zina hatari ya kuchochea mvutano mpana wa kikanda.

“Mtazamo huu wa uchokozi utasababisha misukosuko mikubwa zaidi katika eneo lote na unapaswa kukataliwa kabisa,” alisema.

Kwa sasa Iran inashuhudia wimbi lake kubwa zaidi la maandamano tangu mwaka 2022. Wakati huo huo, Rais wa Marekani Donald Trump amesema Washington inaweza kuingilia kati endapo nguvu zitatumika dhidi ya waandamanaji, jambo linaloongeza hofu ya kuongezeka kwa mvutano na mgogoro zaidi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#