Dollar

42,8555

0.06 %

Euro

50,6985

0 %

Gram Gold

6.194,0500

0.02 %

Quarter Gold

10.244,0200

0.38 %

Silver

99,6800

1.2 %

Mchakato wa kuchunguza na kutathmini vifaa hivi umeanza, amesema Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Yerlikaya.

Uturuki yatangaza kupatikana kwa kisanduku cheusi cha ndege iliyomuua Mkuu wa Jeshi wa Libya

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Ali Yerlikaya, ametangaza kupatikana kwa kisanduku cheusi (Black box) na kinasa sauti cha rubani mapema siku ya Jumatano kutoka kwenye mabaki ya ndege binafsi iliyoanguka karibu na Ankara, Uturuki, usiku wa Jumanne.

Mkuu wa Jeshi wa Libya na watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo wamefariki dunia.

“Kutokana na kazi zilizofanywa katika eneo la tukio na maafisa kutoka Kituo cha Uchunguzi wa Usalama wa Usafiri wa Wizara ya Uchukuzi na Miundombinu, kinasa sauti cha ndege kilipatikana katika eneo la mabaki saa 8:45 usiku, na kisanduku cheusi kimepatikana saa 9:20 usiku,” alisema Waziri huyo.

Waziri huyo aliongeza kwamba mchakato wa kuchunguza na kutathmini vifaa hivi umeanza.

Jumla ya watu 408 wamekuwa wakifanya kazi katika eneo hilo wakitumia magari 103 na ndege 7.

Wajumbe 22 kutoka Libya – ikiwa ni pamoja na familia watano wa waliokufa, wawakilishi wa Wizara ya Ulinzi na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani – wamewasili Ankara, alisema Yerlikaya.

“Sisi pia tuna hamu sana kujua sababu ya ajali, lakini data hii itabaini sababu, na mamlaka itashiriki matokeo na nyinyi,” alisema.

Waziri huyo pia alitoa salamu za rambirambi kwa familia wa waliofariki dunia na kwa serikali na wananchi wa Libya, akieleza tukio hilo kama “ajali ya kusikitisha.”

Yerlikaya hapo awali amesema ya kwamba mabaki ya ndege ya binafsi ya aina ya Falcon 50, iliyotokea kutoka Uwanja wa Ndege wa Esenboga Ankara kuelekea Tripoli, yalipatikana vikosi vya usalama vya Uturuki takriban kilomita 2 kutoka kusini mwa kijiji cha Kesikkavak katika wilaya ya Haymana.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya ilitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#