Ufaransa yaishutumu Iran kwa kushambulia mifumo ya majokofu katika maduka
Ufaransa imeishutumu Walinzi wa Mapinduzi wa Iran kwa kufanya mashambulizi ya kimtandao na kutishia kuweka vikwazo zaidi kutoka Umoja wa Ulaya, huku ikimwita balozi wa Iran kwa mashauriano kufuatia mashambulizi hayo.
9 Novemba 2026
JD Vance anaongoza juhudi za kimya kimya kwa ajili ya makubaliano mapya ya Marekani na Iran
Axios inataja vyanzo vinavyosema kuwa Vance amekuwa akizungumza na wapatanishi, wakiwemo Qatar na Pakistan, kwa wiki mbili zilizopita ili kufikia makubaliano, na kuongeza kuwa wajumbe Witkoff na Jared Kushner walihusika.
8 Novemba 2026
Hegseth anashikilia msimamo wake kuhusu vita dhidi ya Iran, huku Vance na Trump wakivilaumu
Mkuu wa Pentagon, Pete Hegseth, anaapa kupinga jitihada za Bunge la Marekani za kutaka kumuondoa madarakani, na anatetea vita vya Marekani dhidi ya Iran — hatua ambayo Makamu wa Rais JD Vance anasema ilisababisha Chama c
7 Novemba 2026
Rais wa Israel kutangaza siku ya Jumapili atakayeunda serikali mpya nchini humo
Rais Isaac Herzog anafanya mashauriano na vyama vya kisiasa kufuatia uchaguzi wa tarehe 27 Oktoba, ambapo hakuna aliyepata wingi wa kura kati ya Netanyahu wala Eisenkot.
6 Novemba 2026
Panya buku mwenye kilogramu 30 agundulika Thailand
Mnyama huyo, alikuwa na uzani wa kilogramu 30, zaidi ya nusu ya uzito wa mnyama aina ya ngekewa.
5 Novemba 2026
Kiongozi wa upinzani nchini Israel aondoa uwezekano wa kuunda serikali ya umoja na Netanyahu
Yair Lapid anasema kuendelea kwa Netanyahu madarakani kunahatarisha usalama, demokrasia na hadhi ya kimataifa ya Israel.
4 Novemba 2026
Tangazo · 970 × 250
Trump: Vita dhidi ya Iran vilichangia kushindwa kwa chama cha Republican katika uchaguzi
"Nadhani sehemu ya sababu ilikuwa ni Iran, lakini wakati huohuo, watu walielewa umuhimu wa hatua nilizochukua kuhusu Iran," alisema Trump.
4 Novemba 2026
Wapiganaji wa Iran wadai kushambulia droni mbili za Marekani kwenye Mlango Bahari wa Hormuz
Hata hivyo, serikali ya Marekani haijasema chochote kuhusiana na madai hayo ya Iran.
3 Novemba 2026
Ajali ya helikopta juu ya Mlima Everest yaua mtalii wa kihindi
Helikopta hizo mbili, moja ikimilikiwa na kampuni ya Fishtail Air na nyingine na Air Dynasty, ziligongana wakati wakati zikijaribu kutua katika eneo lililojaa theluji katika wilaya ya Solukhumbu, mapema Jumanne.
3 Novemba 2026
Putin amuahidi Ruto kukomesha usajili wa Wakenya katika jeshi la Urusi
Ruto anasema Rais wa Urusi Putin amekubali kuwezesha kurejea kwa Wakenya waliosajiliwa.
31 Oktoba 2026
Putin asema Urusi ni mshirika bora kwa Afrika kuliko nchi zenye historia ya ukoloni
Rais Vladimir Putin anaishutumu nchi za Magharibi kwa kuendelea kujaribu kunyonya rasilimali za bara la Afrika na kutumia madeni kama njia ya kukwamisha maendeleo yake.
29 Oktoba 2026
Netanyahu aongoza, hatima ya kuunda serikali bado haijulikani
Matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Israel yanaonyesha chama cha Likud kinachoongozwa na Benjamin Netanyahu kikiongoza. Mpinzani wake wa chama cha Yashar cha Gadi Eisenkot akishika nafasi ya pili.
28 Oktoba 2026
Rais Lula wa Brazil atimiza miaka 81, aahidi kufanya kazi saa 24
Alipoulizwa kuhusu umri wake, Lula aliweka bayana kuwa, yuko vizuri kiafya, akiendelea kufanya mazoezi ya mwili kama kawaida.
27 Oktoba 2026
Lieberman ataka Netanyahu achunguzwe kwa tuhuma za uhaini kuhusiana na vita dhidi ya Iran
Avigdor Lieberman amemtuhumu waziri mkuu kwa kuwashinikiza maafisa wa usalama kuchukua hatua zinazoweza kusababisha makabiliano na Iran kabla ya uchaguzi.
27 Oktoba 2026
Rais wa Brazil Lula da Silva apata ushindi wa kihistoria wa muhula wa 4 dhidi ya Flavio Bolsonaro
Luiz Inacio Lula da Silva amepata asilimia 51.76 ya kura zilizopigwa duru ya pili, na kuwa wa kwanza kushinda baada ya kushindwa katika duru ya kwanza
26 Oktoba 2026
Maandamano Ufaransa yakigeuka kuwa ya vurugu, huku maelfu wakikamatwa katika miji tofauti
Makumi ya maelfu ya maafisa wa usalama wametumwa katika mitaa ya Ufaransa kufuatia ripoti za uporaji na vurugu zilizoenea.
25 Oktoba 2026
Maelfu ya Waisraeli waandamana Tel Aviv kudai kukomeshwa kwa enzi ya Netanyahu kabla uchaguzi
Viongozi wakuu wa upinzani wanaungana na familia katika maandamano yanayodai uwajibikaji na mabadiliko ya serikali, siku chache tu kabla ya kura muhimu katika bunge la Knesset.
25 Oktoba 2026
Papa Leo XIV aharisha ziara ya Assisi kwa ushauri wa madaktari
Vatican imesisitiza kuwa, shughuli zote za kiongozi huyo, sasa zitafuata ushauri na maelekezo ya madaktari wakati anapoendela kupona baada ya upasuaji wake.
23 Oktoba 2026
Marekani yawaagiza wanadiplomasia wake na familia zao kuondoka nchi za Ghuba
Marekani imechukua uamuzi huo kutokana na uwezekano wa kurejea kwa mapigano, hususan dhidi ya wapiganaji wa Houthi nchini Yemen, kwa mujibu wa ripoti za mashirika ya habari ya AFP na Reuters, zilizonukuu maafisa wanayofa
22 Oktoba 2026
Trump asema Marekani haijadiliani na Iran, aashiria kuwashughulikia 'hivi karibuni'
Matamshi ya Rais wa Marekani yanajiri wakati gazeti la The New York Times likiandika kuwa majeshi ya Marekani na Israel yameandaa mpango wa kufanya mashambulizi mengine baada ya uchaguzi wa Marekani wa nusu muhula.
22 Oktoba 2026
Iran kuzindua bomu lake kubwa zaidi “father of all bombs”
Msemaji wa Jeshi la Mapinduzi ya Iran (IRGC) hajatoa maelezo zaidi kuhusu silaha hiyo, siku chache baada ya Rais Donald Trump kudokeza uwezekano wa kutumia bomu la Marekani linalojulikana kama “mother of all bombs” dhidi
21 Oktoba 2026
Uturuki, Qatar, Indonesia na Pakistan zasaini makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi ya 'Badr'
Mkataba huo wa makubaliano unalenga kuongeza uzalishaji wa vifaa vya kijeshi, kuimarisha uwezo wa ulinzi na kupanua ushirikiano katika mafunzo, utafiti na maendeleo.
21 Oktoba 2026
Uingereza kupeleka ndege za kivita Saudi Arabia kuilinda dhidi ya mashambulizi ya Wahouthi
Uamuzi huo unakuja wakati mashambulizi ya wapiganaji wa kundi la Houthi yakiongezeka, huku Uingereza ikiimarisha msaada wake wa kijeshi wa kujihami kwa Saudi Arabia kufuatia mashambulizi mapya.
20 Oktoba 2026
Makamu wa Rais wa Ufilipino, Sara Duterte apinga kung’olewa madarakani
Mwanasiasa huyo, aliituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kumtumia kama chambo, kuhalalisha usalama wa kitaifa.
20 Oktoba 2026