Hata hivyo, serikali ya Marekani haijasema chochote kuhusiana na madai hayo ya Iran.

Wapiganaji wa Iran wadai kushambulia droni mbili za Marekani kwenye Mlango Bahari wa Hormuz

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limedai kutumia mifumo yake ya ulinzi wa anga kulenga na kuzidondosha droni mbili za Marekani aina ya LUCAS, katika eneo lililo karibu na Mlango Bahari wa Hormuz.

Wakilinukuu shirika la habari la Iran la Fars, IRGC wamedai kuzishambulia droni baada ya kuzibaini zikiwa angani.

Hata hivyo, serikali ya Marekani haijasema chochote kuhusiana na madai hayo ya Iran.

Madai hayo yanakuja huku kukiwa na ongezeko la mvutano kati ya Iran na Marekani, toka kuanza kwa vita vya Marekani-Israel dhidi ya Iran, Februari 28 mwaka huu.

TRT Afrika / AA — TRT Afrika / AA

#