Mnyama huyo, alikuwa na uzani wa kilogramu 30, zaidi ya nusu ya uzito wa mnyama aina ya ngekewa.
Visukuku vya panya buku mkubwa, anayekadiriwa kufikia uzito wa kilogramu 30, vimegundulika nchini Thailand, ambako inadaiwa kuwa mnyama huyo aliishi miaka milioni 35 iliyopita.
Taarifa za ugunduzi wa panya huyo, zilichapishwa siku ya Jumatano na jarida moja la kisayansi nchini Thailand.
Mwanajiolojia kutoka Idara ya Madini ya Thailand, Pannipa Tian, alidai kushangazwa na mabaki ya panya huyo, wakati wa ugunduzi wake.
"Kwa mara ya kwanza nilidhani ni mfupa mkubwa tu, kabla ya kumuonesha mwenzangu ambaye alinieleza kuwa yalikuwa ni mabaki ya panya mkubwa,” alieleza.
Mnyama huyo, alikuwa na uzani wa kilogramu 30, zaidi ya nusu ya uzito wa mnyama aina ya ngekewa.
TRT Afrika / AFP — TRT Afrika / AFP
Picha: Others
