Mwanasiasa huyo, aliituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kumtumia kama chambo, kuhalalisha usalama wa kitaifa.

Makamu wa Rais wa Ufilipino, Sara Duterte apinga kung’olewa madarakani

Makamu Rais wa Ufilipino, Sara Duterte amedai kuwa, upande wa waendesha mashtaka wa nchi hiyo, wameshindwa kutoa ushahidi wenye kuhalalisha kuondolewa kwake madarakani.

"Baada ya Baraza la Wawakilishi kushindwa kuthibithisha pasi shaka kuwa nastahili kung’olewa madarakani," alisema Duterte, ambaye ni binti wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Rodrigo Duterte.

Katika hatua nyingine, mwanasiasa huyo, aliituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kumtumia kama chambo, kuhalalisha usalama wa kitaifa.

"Wote tu mashuhuda wa namna serikali inavyotumia kila njia kunishusha chini," alieleza.

 

#