Helen Haines, anadaiwa kuwa katika hali mahututi katika hospitali ya Alfred iliyoko Melbourne, ambako madaktari wanaendelea kupambania uhai wake.
Mbunge mmoja nchini Australia, amepoteza mguu wake, baada ya kugongwa na gari, nje ya ofisi yake katika eneo la Wangaratta, Victoria.
Helen Haines, anadaiwa kuwa katika hali mahututi katika hospitali ya Alfred iliyoko Melbourne, ambako madakatari wanaendelea kupambania uhai wake.
Siku ya Jumanne, bunge la Australi, liliandaa kikao maalumu, ambapo serikali na wapinzani, walitumia fursa hiyo kulaani tukio hilo.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Anthony Albanese alimuelezea Haines kama mtu aliyejizolea heshima ndani ya bunge la nchi hiyo.
Kwa upande wake, kiongozi wa upinzani Angus Taylor ameshtushwa na tukio hilo, akitoa wito wa kukomeshwa kwa vurugu na za kisiasa nchini humo.
Naye Spika wa bunge la nchi hiyo, Milton Dick, ametoa rai kwa wanasiasa nchini humo, kuheshimiana na kupendana, licha ya tofauti za kisiasa.
