Sport
Dollar
40,2851
0.08 %Euro
46,8742
-0.13 %Gram Gold
4.320,9100
-0.26 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Wanajeshi wanaripoti makabiliano makali na wapiganaji wa RSF, huku makombora kwenye kambi ya wakimbizi yakiwaua raia 8, kulingana na chanzo cha matibabu.
Jeshi la Sudan lilitangaza Jumatano kwamba lilizima shambulio la Vikosi vya RSF kwenye enelo la El-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.
Ilisema wanajeshi kutoka Kitengo cha 6 pamoja na vikosi vya washirika "walisababisha hasara kubwa ya watu na vifaa" kwa wapiganaji wa RSF.
Wakati huo huo, kamati za matibabu ziliripoti kuwa raia wanane waliuawa katika shambulio la mizinga la RSF kwenye kambi ya Abu Shouk kwa wakimbizi wa ndani katika jiji hilo.
Chumba cha dharura katika kambi hiyo kilisema katika taarifa kwamba eneo hilo lilikumbwa na "mashambulizi makali leo yaliyotokana na vikosi vya RSF kwa kutumia mizinga mikubwa.
Imeongeza kuwa shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu wanane, na kujeruhi wengine kadhaa pamoja na uharibifu wa nyumba zilizoko ndani ya kambi hiyo.
Hadi sasa RSF haijatoa taarifa kuhusu tukio hilo.
El-Fasher ni kitovu muhimu cha oparesheni za kibinadamu huko Darfur lakini imekuwa chini ya mzingiro mkali wa RSF na mapigano ya mara kwa mara kwa zaidi ya mwaka mmoja, licha ya juhudi za kimataifa za kutatua makubaliano ya kibinadamu na kuruhusu utoaji wa misaada, ambayo hadi sasa imeshindwa.
Jeshi na RSF wamekuwa wakipigana vita tangu Aprili 2023 ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000 na wengine milioni 14 kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa na mamlaka za mitaa.
Hata hivyo utafiti kutoka vyuo vikuu vya Marekani unakadiria idadi ya vifo kuwa karibu 130,000.
Comments
No comments Yet
Comment