Dollar

40,3076

0 %

Euro

47,0965

0.11 %

Gram Gold

4.335,2200

0.07 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Serikali ya Eswatini imethibitisha kuwa wafungwa watano waliofukuzwa Marekani wamewasili katika nchi hiyo, ikisema hawana hatari yoyote kwa raia wao.

Eswatini inasema wafungwa waliofukuzwa Marekani siyo tishio kwa umma

Serikali ya Eswatini imethibitisha kuwa wafungwa watano waliofukuzwa Marekani wamewasili katika nchi hiyo.

“Ni kweli,wafungwa watano sasa hivi wako katika jela kadhaa wakiwa peke yao, sehemu ambayo wafungwa kama hao wanawekwa," kaimu msemaji wa serikali Thabile Mdluli alisema katika taarifa siku ya Jumatano.

Aliwahakikishia raia wa Swazi kuwa wafungwa hawana tishio lolote kwa nchi yake na wananchi wake.

“Serikali inafahamu kuhusu wasiwasi uliopo juu ya kupelekwa kwa nchi ya tatu kwa wafungwa kutoka Marekani hadi katika Mamlaka ya Eswatini."

'Tathmini ya kina kuhusu hatari'

“Mpango huu ni matokeo ya majadiliano ya miezi mingi yaliyohusisha serikali ya Marekani. Serikali hizi mbili zitashirikiana na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) kuhakikisha kuwa wafungwa hawa wanapelekwa katika nchi zao za asili. Majadiliano hayo yalizingatia kila njia, ikiwemo tathmini ya kina kuhusu hatari na kwa makini kuzingatia usalama na ulinzi wa raia wetu," Mdluli alisema.

Alisema Eswatini na Marekani imekuwa na uhusiano mzuri kwa kipindi cha zaidi ya miongo mitano, na kila makubaliano yanafanywa makini na kwa kuzingatia, tukiweka maslahi ya mataifa yote mawili kwanza.

“Tukiwa kama wanachama wa dunia inayozingatia uadilifu, Eswatini inaheshimu makubaliano na itifaki ya kidiplomasia kuhusu kuwapokea watu, kuhakikisha utaratibu umefuatwa na kuheshimu haki za binadamu,” alisema.

Ubalozi wa Marekani nchini Eswatini umetoa taarifa iliyolenga kuondoa hofu kwa umma kuhusu wafungwa hao.

'Watu hao ni makatili'

Msemaji wa Ubalozi Carly Van Orman amethibitisha kuwa waliofukuzwa Marekani wako chini ya ulinzi ya mamlaka ya Eswatini.

“Mamlaka husika zinahakikisha kuwa kuna usalama na maslahi ya hawa watu kulingana na sheria za taifa huru la Eswatini na utaratibu wa kimataifa,” alisema.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani ilisema siku ya Jumanne kuwa ndege iliyokuwa imebeba wahamiaji kutoka nchi tofauti ilituwa Eswatini katika hatua iliyofuata hukumu ya Mahakama ya Juu ya Marekani kuondoa vikwazo vya kuwaondoa wahamiaji hadi katika nchi ya tatu.

“Ndege ya kwenda nchi ya tatu Eswatini Kusini mwa Afrika imefika. Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu hao waliokuwa makatili kiasi cha nchi zao kukataa kuwapokea tena," msemaji Tricia McLaughlin alisema.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#