Sport
Dollar
40,3098
0 %Euro
46,9988
-0.05 %Gram Gold
4.325,1900
-0.16 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Erdogan na Mohammed bin Zayed wameshuhudia utiwaji saini wa makubaliano ya ushirikiano jijini Ankara, ikiwemo makubaliano kuhusu biashara, ulinzi, utalii, na utafiti.
Uturuki na UAE wamechukuwa hatua kubwa katika kuimarisha ushirikiano wao wa kimkakati, kutia saini makubaliano saba wakati wa ziara ya Rais wa UAE Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan jijini Ankara.
Makubaliano hayo yalikamilishwa siku ya Jumatano mbele ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kufuatia mkutano wa ngazi ya juu kati ya viongozi hao wawili na kikao cha kwanza cha Baraza la Mkakati la ngazi ya juu la Uturuki na UAE.
Akimkaribisha Mohammed bin Zayed na ujumbe wake, Erdogan alieleza ziara hiyo kuwa ni muendelezo wa ushirikiano ulioanzishwa wakati wa ziara yake Abu Dhabi 2023.
“Tuliweka msingi wa ushirikiano wetu wa kimkakati wakati huo — na leo, tunaona matokeo katika karibu kila sekta,” Erdogan alisema.
Kupanua biashara, kuimarisha ushirikiano
Akieleza kuhusu kuimarika kwa uhusiano wa kiuchumi, Erdogan alieleza kuhusu kuongezeka kwa viwango vya biashara: “Miaka michache iliopita, tulikuwa tunajiuliza kama biashara ya dola bilioni 10 inawezekana. Sasa, tunalenga kupita dola bilioni 20 mwaka huu na baadaye kufika dola bilioni 40.”
Makubaliano hayo ni ya sekta mbalimbali, ikiwemo ulinzi, uwekezaji, teknolojia, nishati, utalii, na upatikanaji wa chakula cha kutosha. Kuna MoU iliyotiwa saini kuhusu ushirikiano wa uwekezaji katika sekta ya utalii na hoteli, huku mengine yakiwa kwenye sekta ya dawa, uzalishaji wa viwandani, kilimo, na chakula.
Ushirikiano katika masuala ya ulinzi pia ulirasimishwa kwa makubaliano ya kulinda taarifa nyeti.
Pande zote mbili zilitia saini makubaliano ya pamoja na kuanzisha makubaliano ya kushirikiana katika utafiti, kusisitiza malengo yao ya kuimarisha utafiti wa kisayansi na teknolojia.
Erdogan anasema viongozi hao pia walijadili masuala muhimu ya kikanda, wakiangazia hasa mzozo unaoendelea huko Gaza.
“Ushirikiano wetu siyo kwa masuala ya uchumi tu — umejengwa kwa makubaliano ya kuangazia changamoto za kikanda,” aliongeza.
Ziara hii inaashiria hatua nyingine ya ushirikiano unaoimarika kati ya Uturuki na UAE,kubadilisha kile kilichokuwa kinaonekana kama uhusiano wa kidiplomasia ulokuwa na wasiwasi na kuwa ushirikiano mmoja mkubwa katika kanda.
Comments
No comments Yet
Comment