Sport
Dollar
40,2513
0.11 %Euro
46,8787
0.4 %Gram Gold
4.339,6700
0.99 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mkoa wa Kaskazini wa Niassa unaripotiwa kuathirika zaidi
Msumbiji imethibitisha kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya mpox katika muda wa saa 48 zilizopita katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
Kulingana na ripoti ya Kurugenzi ya Kitaifa ya Afya ya Umma iliyotolewa Jumanne, nchi imerekodi idadi ya maambukizi 11, hata hivyo hadi sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa.
Niassa inaripotiwa kuwa mkoa ulioathiriwa zaidi nchini, ikirekodi angalau maambukizi ya watu watano katika saa chache tu.
Gavana wa jimbo hilo, Elina Massengele, aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa afya wameongeza juhudi ili kuepusha kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.
"Tayari tuna idadi ya watu watano hapa. Tulikuwa tuna watatu, lakini idadi inaendelea kuongezeka na bado kuna watu wengi wanaopimwa ambao wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa huo. Tunapaswa kuwa makini na ugonjwa huu, kwa sababu unaweza kuambukizwa," Massengele alisema.
Katika kukabiliana na maambukizi yaliyogunduliwa katika jimbo hilo, maafisa wa afya walisema Wizara ya Afya ya nchi kupitia Kurugenzi ya Kitaifa ya Afya ya Umma na Taasisi ya Kitaifa ya Afya imekusanya timu ya kiufundi kusaidia wagonjwa walioathiriwa.
"Timu hii itafuatilia matibabu na pia kutambua na kuweka watu walioathirikia katika karantini, kuimarisha uchunguzi wa magonjwa na kupunguza usambazaji kwa idadi ya watu," Massengele alisema.
Maambukizi ya kwanza ya mpox nchini yalirekodiwa mnamo 2022 katika mji mkuu wa Maputo.
Mpox ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinaopatikana kwa wanyama, uligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa wanadamu mnamo 1970 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mnamo Agosti 14, 2024, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya umma ambayo inaleta hofu kimataifa kwa mara ya pili.
Hii ilitokana na kuongezeka kwa maambukizi na vifo, haswa aina kali zaidi za Clade I, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchi jirani za Afrika.
Comments
No comments Yet
Comment