Dollar

40,2512

0.11 %

Euro

46,8845

0.42 %

Gram Gold

4.343,0500

1.07 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kenya imetambuliwa kwa uhamiaji wa kila mwaka wa wanyamapori duniani kwa kuwa mwenyeji wa uhamiaji mkubwa zaidi na wa ajabu unaohusisha zaidi ya swala na pundamilia milioni 1.5 wanaovuka mfumo waikolojia ya Serengenti hadi Mara.

Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara, Kenya rasmi katika Kitabu cha Rekodi za Dunia

Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara imejumuishwa rasmi katika Kitabu cha Rekodi za Dunia, Uingereza, yaani World Book of Records Limited, kama tovuti ya "Uhamiaji Mkubwa Zaidi wa Kila Mwaka wa Wanyamapori Duniani."

World Book of Records Limited, Uingereza ni shirika linaloorodhesha na kuthibitisha rekodi za ajabu kote ulimwenguni kwa uthibitisho halisi.

“Tunafurahia kuwaarifu kuwa Hifadhi ya Masaai Mara hongera sana kwa uhamiaji wa kila mwaka wa wanyamapori duniani na kwa kuwa mwenyeji wa uhamiaji mkubwa zaidi na wa ajabu duniani unaohusisha zaidi ya swala na pundamilia milioni 1.5 wanaovuka mfumo ikolojia ya Serengenti hadi Mara,” Santposh Shukla, rais wa shirika hilo amesema katika barua aliyoituma kwa serikali ya Kenya.

“Utambuzi huu wa ajabu unaheshimu umuhimu wa ikolojia ya Massaai Mara na unaangazia mchango wa kipekee wa Kenya katika uhifadhi wa wanyamapori, anuwai ya kimataifa na utalii endelevu wa mazingira,” taarifa ya shirika hilo imeongezea.

Uhamiaji wa nyumbu kwa kawaida hufanyika kati ya mwezi Julai na Septemba, ambapo wanafika Hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara upande wa Kenya kutoka Hifadhi ya Serengeti Tanzania wakivuka mto Mara.

Kati ya Oktoba na Novemba nyumbu wanaanza kufanya safari na kuvuka mto Mara tena kurudi Serengeti.

Kati ya Januari na Machi ni wakati wao wa kuzaa katika sehemu ya kusini ya Serengeti na kaskazini mwa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Tanzania.

Serikali ya Kenya imesema utambuzi huu ni hatua ya kihistoria kwa sekta ya utalii na uhifadhi wa Kenya na ni wakati wa fahari kubwa kwa nchi hiyo.

“Sifa hii ya kimataifa inathibitisha kile ambacho tumekuwa tukijua siku zote: Maasai Mara ni maajabu ya asili ya ulimwengu. Huku wakiwa na zaidi ya nyumbu, pundamilia, na swala milioni 1.5 wanapovuka mfumo wa ikolojia ya Serengeti-Mara kila mwaka,” Waziri wa Utalii Rebecca Miano amesema.

“Uhamiaji Mkuu sio tu tukio la kustaajabisha—ni ishara ya kina ya usawa wa ikolojia, ustahimilivu, na muunganiko wa maumbile, ”Miano ameongezea.

Utambuzi huo unakuja huku Kenya inapozidisha juhudi za kuvutia wasafiri wanaojali mazingira na kuongeza uwekezaji katika uhifadhi na mipango ya utalii inayozingatia jamii.

Utambuzi huu unainua zaidi nafasi ya Kenya kama kivutio kikuu cha utalii endelevu na kusisitiza kujitolea kwa utalii unaoongozwa na uhifadhi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#