Sport
Dollar
40,2512
0.11 %Euro
46,9147
0.43 %Gram Gold
4.343,2300
1.07 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Wanajeshi hao walikuwa wakishika doria kando ya barabara kati ya Kiunga na Sankuri katika wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetegwa.
Wanajeshi watatu wa Kenya waliuawa Jumanne na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati gari lao lililipuliwa na kilipuzi mashariki mwa kaunti ya Lamu karibu na mpaka na Somalia, jeshi lilisema Jumanne.
Wanajeshi hao walikuwa wakishika doria kando ya barabara kati ya Kiunga na Sankuri wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetegwa.
"Kwa kusikitisha, wanajeshi watatu mashujaa walikufa kwa majeraha," Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) lilisema.
Taarifa hiyo ilisema wanajeshi waliojeruhiwa walihamishwa hadi katika vituo maalumu vya kijeshi, na walikuwa wanapokea matibabu, bila kutoa maelezo zaidi.
Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zilisema kulikuwa na wanajeshi saba waliojeruhiwa.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa uchunguzi umeaznishwa kufuatia tukio hilo.
Comments
No comments Yet
Comment