Dollar

40,3760

0.14 %

Euro

46,9031

0.06 %

Gram Gold

4.326,7100

0 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kuondoka kwao kunatia ukomo wa miaka 65 wa jeshi la Ufaransa nchini Senegal baada ya Rais Bassirou Diomaye Faye kutaka Ufaransa kuondoa vikosi vyake kutoka nchini humo kufikia 2025.

Ufaransa yawakabidhi Senegal kambi ya mwisho ya kijeshi kuashiria ukomo wao Afrika Magharibi

Siku ya Alhamisi Ufaransa ilikabidhi kambi mbili za jeshi kwa Senegal, kufanya Ufaransa kutokuwa na kambi yoyote ya kudumu Afrika Magharibi na Afrika ya Kati.

Kuondoka huku, ambako kunamaliza kuwepo kwa jeshi la Ufaransa nchini Senegal kwa miaka 65, ishara ya kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa kote barani Afrika, ambapo nchi zilizokuwa chini ya ukoloni zikiwakataa wakoloni wao wa zamani.

Ufaransa ilirudisha kambi ya Geille, ni kambi kubwa zaidi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, na kambi ya jeshi la anga katika uwanja wa ndege wa Dakar, katika sherehe zilizohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Ufaransa na Senegal.

Walijumuisha mkuu wa majeshi ya Senegal Jenerali Mbaye Cisse na Jenerali Pascal Ianni, mkuu wa majeshi ya Ufaransa barani Afrika.

Cisse alisema "malengo mapya" yalikuwa yanaangazia "kutoa mtazamo mpya wa makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama".

Vikosi vya Senegal vilikuwa vinafanya kazi "kupata ujuzi mbalimbali kwa ajili ya kujisimamia wenyewe kimkakati ‘‘, aliongeza.

Wanajeshi karibu 350 wa Ufaransa, wengi waliokuwa na jukumu la kufanya operesheni pamoja na wanajeshi wa Senegal, sasa wanaondoka, kukamilisha mchakato wa miezi mitatu wa kuondoka kabisa ulioanza mwezi Machi.

Kutaka vikosi viondoke

Baada ya kushinda uchaguzi wa 2024 na kuahidi mabadiliko makubwa, Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye alitaka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka kufikia 2025.

Faye amesisitiza kuwa Senegal itaendelea kufanya kazi na Ufaransa.

"Senegal ni nchi huru, nchi inayojitawala wenyewe, na utawala wa nchi hauhitaji kuwepo na kambi za kijeshi katika nchi huru," Faye alisema mwishoni mwa mwaka 2024.

Faye pia alitaka Ufaransa kuomba radhi kwa ukatili wakati wa enzi za ukoloni, ikiwemo ukatili wa Disemba 1, 1944, ambapo wanajeshi kadhaa wa Afrika walipigania Ufaransa katika Vita vya Pili vya Dunia.

Kufuatia kujiondoa huku kwa wanajeshi Alhamisi, ni Djibouti peke yake ambapo kutakuwa na kambi ya kijeshi ya Ufaransa. Ufaransa inapanga kutumia kambi ya Djibouti, kwa kuweka wanajeshi 1,500, na kufanya kuwa makao makuu yao ya kijeshi barani Afrika.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#