Sport
Dollar
40,3657
0.1 %Euro
46,9493
0.05 %Gram Gold
4.319,0200
-0.18 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Taasisi ya kupambana na ufisadi nchini Ghana imemshtaki aliyekuwa mkuu wa shirika la kuratibu sekta ya mafuta na wengine sita kwa kuhusika na madai ya ufisadi wa dola milioni 28.
Taasisi ya kupambana na ufisadi nchini Ghana ilisema siku ya Alhamisi kuwa ilimshtaki aliyekuwa mkuu wa shirika la kuratibu sekta ya mafuta na wengine sita kwa madai ya ufisadi wa dola milioni 28 na utakatishaji fedha.
Hii ni hatua ya hivi karibuni katika kampeni aliyozindua Rais John Mahama mapema 2025 kupambana na ufisadi na kurudisha fedha za umma zilizofanyiwa ubadhirifu.
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Maalum inasema iliwasilisha mashtaka 25 dhidi ya Mustapha Abdul-Hamid, aliyekuwa mkuu wa Mamlaka ya Taifa ya Petroli, pamoja na wengine sita na makampuni matatu.
Mashtaka hayo, ambayo yanajumuisha ulaghai wa afisa wa umma na utakatishaji fedha, yanahusishwa na kile kilichotajwa kuwa "njama kubwa ya ufisadi ... iliyoanzishwa na Abdul-Hamid" kati ya 2022 na Disemba 2024.
'Hajawahi kupokea rushwa'
Abdul-Hamid, ambaye anashtumiwa kwa kupokea dola milioni 2.3 moja kwa moja na kufaidika kutokana na njama kubwa ya dola milioni 28, amekanusha madai hayo.
Madai ya kuendesha kampuni za shell
Watu wawili wanashtumiwa kwa kukusanya fedha kinyume cha sheria kutoka kwa makampuni ya masoko ya mafuta na wachukuzi na kutakatisha fedha hizo kupitia kampuni za shell.
Kampuni hizo zilidaiwa kutumiwa "kununua na kujenga nyumba, kununua malori na kufanya biashara za usambazaji wa mafuta, na kujenga vituo vya mafuta," Mwendesha Mashtaka alisema.
Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni moja hajulikani aliko.
Rais Mahama, ambaye alirudi madarakani mwezi Januari, ameahidi kurejesha maadili katika taasisi za umma na kurejesha fedha zilizoibiwa.
Tangu kuzindua kampeni ya kupambana na ufisadi, watu kadhaa wamekamatwa au kushtakiwa, huku wengine bado wanachunguzwa.
Comments
No comments Yet
Comment