Dollar

40,4053

0.12 %

Euro

47,0250

0.23 %

Gram Gold

4.333,8400

0.17 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais Erdogan amelaani uchokozi wa Israel kwa Syria, na kuonya dhidi ya kanda kuungana na Israel, na kusisitiza kuwa Uturuki itaunga mkono umoja wa Syria.

Erdogan aonya hatua za Israel zinaweza kuhatarisha kanda nzima, na 'kuwasha moto duniani'

Israel ni taifa lisilo heshimu sheria, linavunja sheria, halina ustaarabu, jeuri, na la kigaidi ambalo linatumia matatizo katika kanda kuhalalisha hatua zake, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema, akilaani uchokozi unaoendelezwa na Israel dhidi ya nchi majirani.

Akizungumza baada ya mkutano wa baraza la mawaziri jijini Ankara siku ya Alhamisi, rais wa Uturuki alilaani vikali mashambulizi yanayoendelea ya Israel kwa Syria na kote katika kanda, akionya kama uchokozi wa Israel hautozuiliwa basi utasababisha mzozo mkubwa zaidi.

“Israel imekuwa ikitumia jamii ya Druze kama kisingizio cha kufanya uhalifu wake nchini Syria katika siku mbili zilizopita,” Erdogan amesema. “Kwa sasa, tatizo kubwa katika kanda yetu ni uchokozi wa Israel. Kama katili huyu (Israel) hatozuiwa sasa, itasababisha hali mbaya zaidi katika kanda yetu na dunia nzima.”

Kuendelea kuunga mkono uhuru wa mipaka ya Syria

Erdogan amesisitiza kupinga kwa Uturuki kwa majaribio yoyote ya kuigawanya Syria, akisisitiza msimamo wa muda mrefu wa nchi yake kwa kuendelea kuunga mkono umoja wa mipaka ya nchi hiyo ambayo imekuwa vitani. 

“Hatukuidhinisha kugawanywa kwa Syria jana, na bila shaka hatutofanya hivyo leo au kesho,” alisema.

Rais wa Uturuki pia alionya kuhusu mataifa mengine katika kanda dhidi ya kujiunga na Israel, akieleza miungano kama hiyo huwa inatibuka. 

“Wale wanaoingia kisimani na kamba ya Israel hivi karibuni au baadaye watagundua wamefanya makosa makubwa sana,” alisema. “Wale wanaotegemea Israel hivi karibuni au baadaye watagundua wamefanya makosa makubwa sana.”

'Syria yenye usalama ni kanda yenye usalama'

Alisisitiza kuwa mustakabali wa Syria unahusiana moja kwa moja na usalama wa kanda nzima. 

“Syria iliyo salama italeta usalama kwa mataifa jirani ; la sivyo, kila mmoja atabeba mzigo wa tatizo hili,” alisema. “Tunafuatilia kwa karibu yanayoendelea nchini Syria, kuendeleza mawasiliano na wenzetu, na tutaendelea kufanya hivyo.”

Matamshi ya Erdogan yanakuja huku kukiwa na wasiwasi kimataifa kuhusu uchokozi wa hivi karibuni wa Israel kusini mwa Syria, hasa katika maeneo ambayo ni makazi ya jamii ya Druze. 

Maneno makali ya kiongozi wa Uturuki yanaashiria wasiwasi mkubwa wa Uturuki kwa kile wanachoona ni muelekeo wa Israel kutatiza usalama katika kanda na kuweka msisitizo wa kusimama na uhuru wa Syria.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#