Dollar

40,2791

0.07 %

Euro

46,8172

-0.27 %

Gram Gold

4.326,2600

-0.14 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Bodi ya Migodi, Petroli na Gesi ya Rwanda (RMB) ilionyesha maeneo 52 yenye uwezo wa kuzalisha madini nchini kote.

Rwanda kutoa leseni kwa wawekezaji wapya wa madini

Serikali ya Rwanda imeidhinisha maombi ya leseni za madini, machimbo na utafiti, sambamba na kuendelea kwa juhudi za kuimarisha uchimbaji madini nchini, kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Uamuzi huo uliowakilishwa kwa taarifa kufuatia mkutano wa Baraza la Mawaziri lililokutana Julai 16 likiongozwa na Rais Paul Kagame.

"Sekta imepata ukuaji mkubwa katika uzalishaji, uwekezaji na ugunduzi wa madini yenye thamani ya juu," taarifa imesema.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu leseni hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Baraza la Mawaziri lilielezwa kuhusu maendeleo ya sekta ya madini ya Rwanda, ambayo inaendelea kuwa na nafasi ya kimkakati katika kuleta mageuzi ya kiuchumi.

Kwa sasa, sekta ya madini ndiyo chanzo kikuu cha Rwanda katika mapato ya mauzo ya nje.

Mwaka 2024, mapato ya mauzo ya madini yalifikia dola bilioni 1.7 (takriban Rwf2.4 trilioni), kuongezeka kwa asilimia 54 kutoka dola bilioni 1.1 mwaka 2023, kulingana na takwimu rasmi.

Serikali inasema inalenga kuzalisha dola bilioni 2.17 katika mauzo ya nje ya madini kwa mwaka ifikapo 2029, chini ya Mkakati wa Pili wa Kitaifa wa Mabadiliko (NST2).

Katika kikao kilichofanyika Julai 15, na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Wabunge waliona ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Katika ripoti hiyo Bodi ya Migodi, Petroli na Gesi ya Rwanda (RMB) ilionyesha maeneo 52 yenye uwezo wa kuzalisha madini nchini kote.

Hata hivyo, ukaguzi ulionyesha kuwa uchunguzi wa kupata taarifa zinazoweza kutegemezwa kwa ajili ya unyonyaji ulifanywa tu kwa 18 kati yao - ikiwakilisha zaidi ya asilimia 34 ya maeneo yaliyolengwa.

Juni 2025 serikali ya Rwanda ilisimamisha utoaji leseni wa biashara ya madini.

Kulingana na bodi ya Madini, Petroli na Gesi nchini humo (RMB), hatua hiyo ilikuwa na nia ya uboreshaji wa kanuni za sekta hiyo.

Migodi iliyo tayari

Tarehe 16 Agosti, 2025 imetengwa kama siku ya mwisho kwa wawekezaji kuwasilisha maombi ya leseni za kufanya kazi katika maeneo 10 yaliyo tayari kuwekeza katika madini au vitalu vya madini kote nchini.

Ili kuruhusu mwekezaji sharti awe tayari kuwekeza kima cha kuanzia dola milioni 1.9 (Rwf2.8 bilioni) kwa shughuli za uchimbaji mdogo na zaidi ya dola milioni 4.8 ( Rwf7 bilioni) kwa miradi mikubwa.

Kuna vitalu nane tayari kwa uchimbaji madini ambavyo ni Rweru, Rweru-Kimvubu, Rugarama, Nduba, Remera, Musenyi, Mamfu-Rwasama, na Juru na vitalu viwili vya kiwango cha kati ambavyo ni Rubiha na Binyeri.

Kulingana na RMB, leseni zinazotolewa kwa ajili ya zabuni ni kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini zinazohusisha madini ya cassiterite, columbite-tantalite (coltan), na wolframite.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#